Bunge Laendelea Kujadili Taarifa Ya LAAC....Mbunge Ashauri Serikali Ianzishe Chuo Cha WIZI
1
May 28, 2020
Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.
Bunge la Bajeti ,mkutano wa 19 kikao cha 38 limeendelea kujadili hoja ya Kamati ya kudumu ya Bunge ya Hesabu za serikali za Mitaa[LAAC] kuhusu ripoti ya Mkaguzi na mdhibiti mkuu wa Hesabu za Serikali[CAG] huku serikali ikishauriwa kuanzisha chuo cha Wizi ili kukabiliana na ubadhilifu wa mali za umma.
Wakitoa michango ya maoni mbalimbali leo Mei,28,2020 juu ya Ripoti ya CAG iliyowasilishwa bungeni jijini Dodoma na kamati ya kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za mitaa[LAAC],Mbunge wa Kahama mjini Mhe.Jumanne Kishimba ameshauri serikali kuanzisha chuo cha Wizi ili kuweza kupambana na ubadhilifu wa mali za umma.
Mbunge wa Ukerewe Mhe.Joseph Mkundi amesema kuna baadhi ya watumishi ngazi ya halmashauri wasiokuwa waaminifu wamekuwa wakitumia Mashine za ukusanyaji mapato[POS] kwa njia ya udanganyifu na kusababisha halmashauri kupata hasara hivyo kuna haja ya kuwafukuza huku Mhe.Hasma Mwilima akishauri namna ya kupata mafunzo Zaidi Wakurugenzi wa halmashauri ili kuweza kupambana na watumishi wasiokuwa waaminifu.
Naibu Waziri wa Kazi ,Ajira na wenye Ulemavu,Mhe.Stella Alex Ikupa amesema serikali ya awamu ya tano imekuwa na mchango mkubwa katika kuwezesha mikopo watu wenye ulemavu,huku Naibu waziri Ofisi ya Rais ,utumishi wa Umma na utawala bora Dkt.Mary Mwanjelwa ametoa pongezi kwa watumishi kufanya kazi bila kuchoka ambapo Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii ,Jinsia,Wazee na Watoto Godwin Mollel akizungumzia suala la tiba asilia aemesema ni suala la kibiblia.
Naibu waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi,Mhe.Agelina Mabula amesema wizara hiyo imesogeza huduma za ardhi ngazi ya mikoa huku Naibu Waziri wa ujenzi na Uchukuzi Elias Kwandikwa akizungumzia suala la mapato Zaidi ya Bilioni 17 hazikwenda kwenye miradi ya maendeleo ambapo Naibu Waziri wa Kilimo Mhe.Omary Mgumba amekiri hoja ya gharama kubwa katika miradi ya Umwagiliaji.
Akijibu hoja ya posho ya Madiwani,Waziri wa Ofisi ya Rais ,Tawala za mikoa na Serikali za Mitaa [TAMISEMI]Seleman Jafo amesema kwa mujibu wa takwimu za hivi karibuni , Zaidi ya Bilioni 10 zimeshalipwa huku Mwenyekiti wa Kamati ya hesabu za serikali za mitaa [LAAC] Vedasto Edgar Ngombale akihitimisha hoja ya kamati kwa kuipongeza serikali kwa kuanza kutekeleza maagizo ya CAG.
MWISHO.
Tags
Asanteni wengine wote, Mada na Rai ya
ReplyDeleteJ4 Kishimba ni ya kuifanyia kazi yeye
hakuiremba katika Uwasilishaji its blunt.
Ni sisi Kuipa jina stahiki na informative . Kama tutaita Fraud Technics studies au Goverment Enhenced
Assets/liability studies.
Mkuchika/Kijazi/Kikwete/Mipango inabidi mkae mlitafakari kwa kina.
Kama alivyosema Jumanne Hili ni swala Geni.
Ukweli ni kwamba huko Duniani katika
corrective institution walio ndani wanalipwa kuandika case studies on
How its Done. Benki na Wizara Husika
wanazifanyia Awareness course na pia kuigiza katika vigezo ktk Uajiri.
J4 ni very innovative cool MP.
Deserves kuwa Consultant as always
he plays outside the box. I reccomend him to be a board member of any smart
city that will be built in our country