Burundi Mambo Yameiva..Wananchi Wasubiria Matokeo ya Uchaguzi


Zoezi la upigaji kura nchini Burundi limemalizika salama na kwa utulivu hapo jana, licha ya fukuto la machafuko ya kisiasa, janga la virusi vya corona huku upinzani nao ukizituhumu mamlaka kwa udanganyifu. Rais Pierre Nkurunziza ambaye serikali yake mara kwa mara imeshutumiwa kwa ukiukaji wa haki, hatimaye ataondoka madarakani baada ya miaka 15.

 Kiongozi wa upinzani, Agathon Rwasa hata hivyo amesema waangalizi wa uchaguzi kutoka chama chake walifukuzwa kwenye vituo vya kupigia kura.

 Rwasa aliliambia shirika la habari la Reuters kwamba itakuwa vigumu kwao kukubaliana na matokeo kwa kuwa pamoja na udanganyifu mkubwa na waangalizi wao kufukuzwa vituoni, hawajaweza kushuhudia zoezi la kuhesabu kura.

Serikali haikuzungumza chochote ilipoombwa kuzungumzia madai hayo.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad