CHADEMA Wamjibu Spika, Wahoji Wakapime Wapi


CHADEMA Wamjibu Spika, Wahoji Wakapime Wapi
CHADEMA kimemjibu Spika Ndugai kwa kumuambia kuwa kama anataka Wabunge warudi Bungeni wakiwa wamepima, basi aseme anataka wakapime wapi kwa kuwa Serikali imepoteza imani na Maabara yake na inaichunguza, na kuongeza kuwa yeye ndiye Spika wa kwanza kulipa posho kwa Mbunge hewa Cecil Mwambe.

Hayo yamebainishwa leo Mei 7, 2020, na Mkurugenzi wa Mawasiliano, Itifaki na Mambo ya Nje wa chama hicho John Mrema, na kusema kuwa si vyema Spika kutoa kauli ya namna ile kwa watu ambao tayari wamekwishajiweka karantini na kudai kuwa kama anahisi Wabunge hao hawako Dodoma wanazurura basi awataje kwa majina.

"Uwezo wa kupima Wabunge si wa chama ni uwezo wa Serikali na Maabara iko moja na inachunguzwa, kwahiyo anataka wakapime wapi ili hali Maabara yenyewe inachunguzwa?, ataje ni nani ambaye anazurura na aseme wapo wapi, ajaribu tu kuwatafuta hapo Dodoma kama hatowaona" amesema Mrema.

Aidha akizungumzia Sakata la Mbunge Cecil Mwambe ambaye alikwishajiuzulu, na jana Spika Ndugai aliagiza Mbunge huyo kurejea Bungeni, Mrema amesema kuwa.

"Nchi hii hatujawahi kuwa na sheria ya mgombea binafasi, Cecil Mwambe alisema hadharani na kupokelewa CCM, nashangaa Spika anapata wapi hayo mamlaka, mbona Wabunge wengine hawarudishi, kama wanaamua kumlipa ni utaratibu wao wa hovyo, tunasubiri tuone kama Spika ana uwezo wa kumrejesha Mwambe uanachama wa CHADEMA" ameongeza.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad