CHADEMA Wataja Sababu Ya Freeman Mbowe Kuitwa Polisi




Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kupitia kwa Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa chama hicho Tumaini Makene, kimesema kuwa Jeshi la Polisi Kinondoni lilimuita Mwenyekiti wa chama hicho Freeman Mbowe, ili kujua alikuwa anataka kuhutubia kitu gani kwa umma.

Makene ameyabainisha hayo leo Mei 15, 2020, na kueleza kuwa baada ya kumhoji kwa muda, hatimaye Jeshi hilo ilipofika majira ya jioni lilimuachia na kuruhusu aendelee na shughuli zake.

"Aliripoti kama ambavyo alipokea wito kutoka kwa RPC Kinondoni, na walitaka kujua sababu ya yeye kutaka kuzungumza na umma na baadaye jioni aliruhusiwa kuendelea na shughuli zake, na suala la mkutano liko pale pale, kwahiyo sasa tunaangalia kwenye hotuba kama kutakuwa na vitu vya kubadilisha ama vibaki vile vile kulingana na wakati na siku" amesema Makene.

Jana Mei 14, 2020, Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe, ilikuwa azungumze na umma mubashara, lakini mkutano wake uliahirishwa baada ya kupokea wito wa Jeshi la Polisi Kinondoni.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad