Chadema: Wenye Ushahidi Ufujaji Fedha Wauweke Hadharani



CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimewataka Wabunge wenye ushahidi juu ya tuhuma za matumizi mabaya ya fedha kuuweka hadharani.

Hayo yamesemwa na Benson Kigaila, Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho Bara, kufuatia wimbi la Wabunge waliotangaza kukihama chama hicho na kudai kwamba Mwenyekiti Freeman Mbowe anatumia vibaya fedha za chama.

Mei 22, 2020 Susan Maselle na Joyce Sokombi, Wabunge Viti Maalumu wa CHADEMA, walitangaza adhima ya kukihama chama hicho na kujiunga na NCCR-Mageuzi na kutoa shutuma kadhaa ikiwamo unyanyasaji wa kingono.

Pia, walidai hakuna mtu anayeruhusiwa kuhoji juu ya matumizi ya fedha za CHADEMA ambapo tuhuma hizo pia ziliwahi kutolewa Bungeni na Spika Job Ndugai na kumtuhumu Mbowe kuwa anawalazimisha wabunge kuchangia fedha hizo.

Wakati huohuo,  Kamati Kuu ya CHADEMA imefanya kikao chake kwa njia ya kidijitali na kujadili mambo mbalimbali ikiwemo maandalizi ya kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Oktoba katika mazingira ya uwepo wa #Corona, kupitia kikao hicho Mbowe kwa niaba ya CHADEMA amewatakia heri ya Eid Al Fitr Waislamu wote.
Tags

Post a Comment

4 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Utafanyaje Zulu a KATIKA SACCOS halafu ukasahau kuwa Mbungo yupo Tena Macho.

    Walioamua kuse a siyo mmoja NI WENGI tuu.

    Utajengaje Mahoteli ya kitalii ili Hali mshahara wako unajulikana??

    Usijifanye Hamnazo Kuna WATU Machizi halafu wamerogwa.

    Lazima uturudishie Maka do Mando yetu. Ubunge ndiyo Mariya Kuyshnehi.

    ReplyDelete
  2. Kigaila, Majambazi 7 wauawa DSM
    Hao w alikuwa wajuaji wameuliwa.

    Sasa naulizia Msambazaji kona Si muuaji pia?

    Kwa hivyo tunaweza kusema pia ni
    JAMBAZI au nakosea?

    Na Genge LA MAJAMBAZI tutaliitaje
    AU Mpaka LIJUALIKALI Aje Atafsiri

    ReplyDelete
  3. Ukicheza karata, huku unayo magarasa wewe ukafikiri NI Turufu

    BASI hata Mrisi hutoki.

    Na ndiyo ilivyokuwaokidiwni yenu.
    Imekula kwenu na wananchi tumesga wasoma sitegemei kama mtarudi Tena Mjengoni Jijini DODOMA.

    Karata ya Koro a imekufilisini vibaya kabisa mnatoka Bina kuonewa huruma. Mtafute AJIRA korokoroni WA kulinda pagale lenu

    JPM Anapuyanga na Tanzania tunapuyanga nyie endeleeni kushanga shanga. Ukitahamaki wewe na M/Kiti mtaishia kucheza draft na bao. Anzeni kuwekeza KATIKA mabirika ya kahawa kijiweni.

    Siasa hamuijui na hamuiwezi imekushindeni. Kwa malumbano Mko vizuri lakini Si kwetu Tanzania.

    Mkatafute PA kujiweka na kujiongeza. Bongo No No Nooooo!!

    ReplyDelete
  4. CHADEMA imekula kwnu Tena kwa kiasi kikubwa kisicho namfano.

    Tumeona kwa marudio mfululizo Usanii wenu wa kutoka BUNGENI na Upingaji wa Miswada ya BAJETI za serikli, za mipango ya Kimikakati ya MAENDELEO.

    Tumeshuhudia jitihada mnazofanya kuhakikisha Chama kilichopo madarakani kwamba kionekane hakimudu Uongozi wa Taifa (Hilo Mlishindwa KATIKA AWAMU HII ya TANO na mmejaribu kujizolea umaarufu na Sifa kwa hoja ambazo, mwisho wa siku zote zikaonekana kuwa Hoja mchwara) mmepiga chini ma Ajenda za kudandia HAZIPO tena Magu kazishughulikia kwa kiasi kikubwa, mkaamua kuhamia TWITA na Fesibuku. ndiyo viwanja vyenu vipya.

    Sitegemei kama Kuna Mtanzania mwenye akili timamu ataitoa hata Robo kura yake kwa Genge hili la Wapinga MAENDELEO.

    WaTanzania WAnacho taka NI MAENDELEO /HUDUMA na Si vinginevyo.

    Sasa Dhuluma na Ujambazi wa Hi Tech mnaoufanya kuwaumiza Wabunge na wa Viti Maalumu ikiwemo Ruzuku Kibindoni Hapo mnachezea Sharubu za Dola.

    Jaji Mtungi / Biswalo/ A.Diwani / ni kwamba mmesha watonya na wao Hivi muda hawato wabeep ila watawapigia na Ngoma itakuwa Tamu. tena Tamu kweli kweli na Zege kwao huya Mbungo Halilazi.

    Tanzania ina Amani tunaomba Ushirikiano wenu Ili tuendelee KUDUMISHA AMANI YETU.

    Vibaraka na Mamluki HATUWATAKI KWETU.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad