China yalaani kitendo cha Marekani kukataa kutoa vibali vya kuingia nchi hiyo wanafunzi wa China




Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China amelaani kitendo cha Marekani kukataa kutoa vibali vya kuingia wanafunzi wa China katika nchi hiyo. 

Zhao Lijian amesema kuwa vitisho vya serikali ya Marekani dhidi ya wanafunzi wa China sambamba na kukataa kuwapatia viza, ni kinyume na uwazi na uhuru ambao Washington imekuwa ikidai kuutekeleza. Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China ameitahadharisha Marekani isijaribu kukiuka kwa namna yoyote haki za wanafunzi wa China, kwa kuwa kitendo hicho kitakuwa ni ubaguzi wa rangi. 



Malalamiko ya Wizara ya Mambo ya Nje ya China yametolewa katika hali ambayo Beijing imekuwa ikilalamikia uingiliaji wa Marekani katika masuala ya ndani ya eneo la Hong Kong na Taiwan, na kuitaka isimamishe uingiliaji wake huo mara moja. Uhusiano wa Washington na Beijing umezidi kuvurugika na kufikia kiwango cha chini kabisa hasa baada ya kuingia madarakani Rais Donald Trump. 


Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad