Corona yaanza kuingia Ikulu ya Marekani, Msaidizi wa Makamu wa rais Mike Pence akutwa na Corona


Msaidizi mwingine mkubwa wa Mike Pence amekutwa na virusi vya corona siku moja baada ya mfanyakazi mmoja wa White house kukutwa na virusi hivyo.



Katibu wa Pence, bi Katie Miller alikutwa ana virusi vya corona siku ya Ijumaa siku moja baada ya rais Donald Trump kutaka wapimwe.

White House ilianza kufanya vipimo vya kila siku kwa ajili ya bwana Pence na bwana Trump, na kudaiwa kuwa tahadhari zote zinachukuliwa ili kumlinda rais.

Vifo vinavyotokana na virusi vya corona vimeongezeka na sasa kufikia zaidi ya 76,000 na huku majimbo yameanza kufunguliwa.

Watu sita ambao wanafanyakazi na Bwana Penceka kwenye waliondolewa ghafla kwenye ndege yake, Air Force 2, baada ya kuwa na safari nje ya Washington, Kamishina ametumia zaidi ya saa moja siku ya Ijumaa wakati akijiandaa kwenda kukutana na viongozi wa dini.

Wafanyakazi ambao waliwasiliana na Bi.Miller hivi karibuni, kwa mujibu wa maofisa wa Marekani.

Rais na Makamu wa rais hawajakutana naye.

Bi. Miller ni mke wa msaidizi wa Trump, Stephen Miller.

Mr Trump visited the WWII memorial in Washington DC on FridayBwana Trump alitembelea eneo la makumbusho ya Vita Kuu ya Pili ya Dunia mjini Washington DC Ijumaa
Wakati wa kikao na Republicans katika White House, bwana Trump aliwaambia waandishi.

“Ni mwanamke mzuri, Katie.”

“Aliwahi kupima muda mrefu na ghafla akapima tena na kukutwa na virusi vya corona.”

Nilipouliza kama kuna uwezekano wa mlipuko wa corona kuzuka katika White House, bwana Trump aliwaambia waandishi: “Kile ambacho mnajhitajika kukifanya ni kuchukua tahadhari kadri muwezavyo.”

Alisema pia , alisahihishwa kwa kutovaa barakoa wakati alipotembelea kumbukumbu za vita ya pili ya dunia kwa sababu wanajeshi wastaafu ambao ni wazee walikuwa mbali naye”.

, “Pamoja na upepo kuwa mkali, bado ingekuwa vigumu sana kwa maambukizi kuwafikia na kwanza nngeshangaa sana,” aliongeza.

Kuonyesha kuwa kila kitu kiko sawa
Rais ameweka wazi kuwa kuwa hapendi jinsi mask inavyomkaa akivaa ndio maana anaepuka kuvaa.

Alisema mwezi uliopita kuwa anaamini kuwa kuvaa barakoa hakukufanyi kuwa kiongozi mzuri duniani zaidi yaw engine.

“Mimi kama rais, waziri mkuu, kiongozi wa kimabavu, mfalme au malkia…. …sijioni hapo mwenyewe, yaani sijioni,” Trump aliwaambia waandishi.

Kwa rais kukataa kuvaa barakoa ni swali zaidi ya mtindo tu.

Ni taarifa ya kisiasa.

Trump na maofisa wengine wa White House waanataka kuwaaminisha watu kwa kuwaonyesha watu kuwa janga la afya linakabiliwa na uchumi utarudi katika hali yake ya kawaida.

Mapema siku ya Ijumaa, Trump alisema kuwa wasaidizi wake wameanza kuvaa barakoa.

Siku moja kabla ilibainika kuwa mmoja wa wanajeshi wa Marekani ambaye anahusika katika chakula cha Rais alikutwa na virusi vya Corona.

Trump anasema kuwa awali vipimo vya mtu huyo vilionyesha kuwa hana maambukizi mara nne mfululizo.

“Hii ndio maana kuwa vipimo sio wakati wote ni jibu, alisema, licha ya kuongeza kuwa wafanyakazi watakua wakipimwa kila siku. “Kupima pekee sio suluhisho”

Awali msemaji wa ikulu ya Marekani Kayleigh McEnany alisifia hatua zinazochukuliwa na ikulu hiyo kuwafanya maafisa kuwa salama.

“Tumechukua hatua madhubuti kumlinda Rais, alisema McEnany.

Siku ya Ijumaa taasisi ya Marekani ya chakula na na dawa (FDA) ilithibitisha kipimo cha kwanza ambacho kinaweza kutumika nyumbani.

Taasisi hiyo inalaumiwa kwa kuruhusu usambaaji wa vipimo kiholela ambavyo baadhi yao vimekua vikitoa majibu ya uongo.

Kwa mujibu wa ikulu ya Marekani, takriban watu 248,000 hupimwa kila siku na mpaka sasa wamepimwa watu milioni 8.1
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad