‘Diamond Anafaa Kunikumbuka pia.’ Babake Platinumz Azungumza Kuhusu Hatua ya Msanii Huyo Kuzisaidia Familia Fukara


Katika video inayosambazwa mtandaoni, babake Diamond anaomba kusaidiwa akisema pia anastahili kunufaika na ukarimu wa mwanawe ambaye ameahidi kuzilipia kodi ya miezi mitatu familia 500  kwa ajili ya janga la corona .

 “ Itakuwa  vyema akanikumbuka. Hatukutani wakati mwingi  isipokuwa wakati wa dharura. Hapo ndio kuna tatizo. Hatuzungumzi sana lakini wakati mwingine huwa nazungumza na Babu Tale. Huwezi kumlazimisha mtu kufanya kitu. Hafai kujitenga kwa muda mrefu hadi kiwango cha kunisahau, mungu husamehe, naye pia anafaa kusamehe. Mimi bado ni babake na anaamini siku moja atakuja hapa kwangu. Hatokuwa na baba mwingine.’ Amesema babake Diamond .

Mwaka jana  Diamond  na babake walikutana na kusameheana katika kituo cha redio cha msanii huyo na hata wakafanya mahojiano ya pamoja. Katika mahojiano ya hivi maajuzi, Mzee Juma alisema hawezi kumlaumu mamake Diamond kwa tofauti kati yake na msanii huyo .

 “ Familia zina mambo mengi na naamini kwamba tulizungumza na kusuluhisha mambo. Yeye ni mtu mzima na mamake hawezi  kumshawishi kufanya vitu. Naamini siku moja atakuja  kugundua kwamba  baba na mama wote ni muhimu.’

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad