Dilunga Afungukia Dili Lake YANGA SC
0
May 10, 2020
Kiungo mshambuliaji wa Simba, Hassan Dilunga, amesema kuwa kwa sasa hafikirii kurejea tena Yanga na akili zake amezielekeza kucheza soka la kulipwa nje ya nchi.
Dilunga ni kati ya wachezaji waliowahi kucheza Yanga na sasa yuko Simba ambako mkataba wake unatarajiwa kumalizika mwishoni mwa msimu huu wa Ligi Kuu Bara.
Kiungo huyo hivi karibuni alikuwa akitajwa kuwaniwa vikali na Yanga ambayo inaelezwa alitengewa dau la Sh Mil 80 ili asaini mkataba wa miaka miwili ya kukipiga Jangwani.
Akizungumza na Championi Jumamosi, Dilunga alisema kuwa ndoto zake zimefanikiwa za yeye kucheza kwenye klabu kubwa hapa nchini za Simba na Yanga, alichobakisha yeye ni kucheza nje ya nchi.
“Ndoto za wachezaji wengi hapa nchini ni kucheza klabu kubwa za Simba na Yanga ambazo mimi pia ilikuwa ndoto zangu ambazo zimefanikiwa kwa kiasi kikubwa kwangu.
“Nimepata taarifa za mimi kutakiwa na timu yangu ya zamani ya Yanga, nilikuwa tayari kurejea huko lakini kwa hivi sasa sitakuwa katika sehemu nzuri ya kurejea huko.
“Ninataka kutimiza malengo yangu ya mimi kucheza nje ya nchi na huu ninaamini ndiyo wakati wangu muafaka wa kwenda huko kucheza kama siyo nchi za Ulaya basi Afrika,” alisema Dilunga.
Tags