Dkt. Abbass: Kiuchumi tuko vizuri ndio maana hatujashusha mishahara ya watumishi kama nchi nyingine


Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbas amesema, Serikali haijaacha kuwalipa watumishi wake katika kipindi hiki cha #CoronaVirus kwa sababu iko vizuri kiuchumi

Ameongeza, “Nchi jirani zimepunguza mishahara lakini kwa Tanzania watu bado wanapata mishara yao tena kwa wakati bila kusheleweshwa”

Amebainisha “Corona imegusa sana uchumi na sekta nyingine mbalimbali lakini hatua tulizochukua kama Tanzania zimetuweka katika nafasi nzuri na kulinda uchumi wetu”

Amesema maambukizi ya #CoronaVirus yamepungua sana, Watu wengi wanapima na amebainisha kuwa takwimu zinaonesha Wagonjwa hawafiki 60 kwa Tanzania

Aidha, vipimo vya sasa vikitoa majibu vinaaminika zaidi kuliko vile vya awali ambavyo vilitoa majibu ya Mapapai na Mbuzi wakiwa wameathirika na virusi hivyo

Amemalizia, “Nchi nyingi zimebadili mkakati wa utoaji taarifa, nyingi zimeacha kutoa taarifa za COVID19. Tumebadili sababu tunaamini Watanzania wameelewa lakini pale kwenye umuhimu tutaendelea kukumbushana”

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad