Donald Trump aiwekea vikwazo China kufuatia sheria yake ya usalama Hong Kong



Rais wa Marekani Donald Trump ametangaza kuweka vikwazo vipya dhidi ya China, akiituhumu tena kuhusika kwa maelfu ya vifo vilivyoptokana na ugonjwa hatari wa Covid-19.

Ametangaza pia kutokubaliana na sheria ya usalama wa China kwa Hong Kong ambayo imeendelea kuzusha wasiwasi mkubwa katika kimbo hilo linalojitawala.

Donald Trump ametekelza vitisho ambavyo amekuwa akitoa kwa siku kadhaa dhidi ya China.

Rais Trump amesema kuwa China imekiuka makubaliano ya uhuru wa Hong Kong kwa kupitisha sheria ya usalama wa Kitaifa. Nakala ambayo inaruhusu kurudi kwa vyombo vya usalama vya China kwa koloni la zamani la Uingereza na ambayo kwa wengi ni tishio kwa uhuru wa eneo hilo.

"Uchina inadai kulinda usalama wa kitaifa. Lakini ukweli ni kwamba Hong Kong ni eneo huru linalojitawala, lenye usalama na ambalolinaloendelea kuistawi kiuchumi na maendeleo mbalimbali. Uamuzi wa Beijing ni hatua ya kurudi nyuma. Uamuzi ambao unaimarisha uwepo wa China kwa mfumo wa usalama kwa eneo ambalo ni uhuru, "Rais wa Marekani amesema.

Uingereza, Japan, Canada, Australia na Marekani zimeelezea wasiwasi wao kuhusu sheria ya usalama wa China kwa Hong Kong. Uingereza imesema sheria hiyo inaweza kukandamiza mamlaka ya ndani ya Hong Kong.

Hisia mbalimbali zinazidi kutolewa kufuatia hatua ya bunge la China kuidhinisha mipango ya sheria tete ya usalama kwa Hong Kong. Waziri Mkuu wa China Li Keqiang amesema sheria hiyo mpya inalenga kuulinda mji wa Hong Kong, lakini Japan, Marekani, Canada, Australia na hata Marekani zimeikosoa hatua hiyo.

Katika taarifa ya nadra, punde tu baada ya sheria hiyo kupitishwa, wizara ya mambo ya nje ya Japan imeutaja mji wa Hong Kong kama mshirika muhimu zaidi. Yoshihide Suga ambaye ni waziri mwenye hadhi ya juu katika baraza la serikali la Japan amesema.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad