Fahamu Kuhusu Historia ya Bibi Titi
0
May 20, 2020
Bibi Titi Mohammed alizaliwa Juni, 1926 na moja ya kumbukumbu tulinayo ya Mwanaharakati huyu katika Taifa letu ni Mtaa na Barabara ya Bibi Titi uliopo jijini Dar es salaam
Bibi Titi aliingia katika siasa kwa kushawishiwa na Schneider Plantan na yeye ndiye alikuwa muasisi wa Umoja wa wanawake Tanganyika (UWT) ulioundwa rasmi Mwaka 1963
Bibi Titi alikuwa na maneno makali dhidi ya ukoloni na alikuwa na ushawishi mkubwa. Akiwa na miaka 16 tu alikuwa mmoja kati ya wanawake wachache walioaminiwa katika kuongoza mapambano dhidi ya udhalimu waliokuwa wakifanyiwa Watanganyika
Baada ya Uhuru alichaguliwa kushika nafasi mbalimbali za uongozi ikiwemo Ubunge, Uongozi wa Wilaya ya Rufiji na Mufindi, Rais wa Umoja wa wanawake Tanganyika(UWT) na baadae Waziri
Mwaka 1968 ,Bibi Titi pamoja na aliyekuwa Waziri wa ulinzi, Michael Kamaliza walikamatwa na kuhusishwa na matukio ya uhaini na wakahukumiwa kifungo cha maisha lakini mwaka 1972 waliachiwa kwa msamaha wa Rais
Alifariki Novemba, 2000 baada ya kusumbuliwa na matatizo ya moyo na kupelekwa katika hospitali ya Net Care, Afrika Kusini kwa ajili ya matibabu
Tags