Fahamu Matumizi ya Overdrive (OD) Kwenye Magari ya Automatic

Overdrive (OD) ni gia katika mfumo wa gari ambayo huifanya gari kuwa katika spidi kubwa huku mzunguko wa injini ukiwa mdogo. Kwa lugha rahisi, OD ni gia ya mwisho inayokupa mwendokasi. OD hukupa mwendo wa kasi, uliotulia lakini kwa mzunguko mdogo wa injini (revolutions per minute rpm). Hii hukuwezesha kuwa na matumizi madogo ya mafuta pengine kwa kasi zaidi.

Overdrive ni kama gia ya ziada inayokupa mizunguko mingi ya driving shaft kwa mizunguko michache ya injini yako. Unapaswa kuitumia ukiwa unatembea mwendo mkubwa. Faida zake utatumia mafuta kidogo, maana gari inakwenda kasi kwa mizunguko michache ya injini.

Mfano katika gari ya kawaida yaani 180km/h ili ufikishe spidi 120 basi RPM inaweza ikawa 4000rpm katika barabara ya tambarare. Lakini ukiweka overdrive unaweza kutembea spidi hiyo hiyo kwa rpm 2000 katika barabara ya tambarare.

Utatambuaje kama Overdreive (OD) ipo on au off?

Pindi uonapo kitaa cha overdrive kwenye dashboard ya gari yako, inamaanisha kuwa overdrive ipo off na pindi kitaa hicho kisipoonekana basi tambua kuwa overdrive ipo on. Overdrive imewekwa kama chaguo (option) la kutumia wakati ukiwa unatembelea spidi chini ya 60km/h.

Unaweza kutumia ukiwa unataka kuipita gari nyingine, mathalani kwenye milima ambapo gari yako inakuwa imepunguza nguvu, hivyo unaweza kuiweka off (hapa unakuwa kama umerudisha namba 4) na injini itabadili kasi ya mzunguko, utaiweka ukishamaliza tena matumizi yake.

Eneo lingine, ni mara gurudumu la gari lako linapopasuka. Ikitokea hivyo, unaweza kuondoa OD, huku ukiwa umeacha kukanyaga pedeli ya mafuta, kwa maana ndiyo utakuwa unaomba mwendo upungue pasi na kukanyaga breki. Katika hali kama hii, utakuwa umesaidia kupunguza mwendo wa gari wakati ukithibiti muelekeo wa gari pia.

Katika hali kama hii huwa wanakanyaga breki. Kufanya hivi ni hatari, maana unasimamisha kabisa mwendo wa gurudumu lililopasuka, na matokeo yake mwendo wa gari, badala ya kwenda mbele, itajaribu kutii amri ya gurudumu linalogomea gari kwenda mbele na kuamua kwenda upande wa gurudumu lililopasuka, nikiwa na maana kwamba hapo gari itakuwa inaacha njia na au kupinduka.

Kwa giaboksi zenye kujibadili zenyewe, ni vema basi tukaziacha OD zijiendeshe zenyewe, maana kuziondoa hatari yake ni kuwa unaweza kusahau kuiweka tena unapokwenda zaidi ya km 70 kwa saa, mfano barabara ya Nyerere, na kusababisha matumizi makubwa ya nishati ya kuendeshea mtambo.
Kitaa cha Overdrive kikiwa hakionekani kwenye dashboard yako maana yake Overdrive ipo Automatic au on na hivyo ndivyo inavopendekezwa na wataalam gari iwe automatic pindi upo mjini na unatembelea speed tofauti (sometimes less or more than 60)..kwa vile overdrive inatumia gia kubwa na mwendokasi chini ya 60km kwahiyo unaweza kutumia wakati unashuka milima mikubwa.
-Mwananchi

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Mada nimeipenda, naomba msaada katika eneo moja. Nikiwa ktk rough road O/D huwaka kama indicator(huwaka na kuzima kama indicator) vipi Gari ipo vizuri?

    ReplyDelete
  2. Mada nimeipenda, naomba msaada katika eneo moja. Nikiwa ktk rough road O/D huwaka kama indicator(huwaka na kuzima kama indicator) vipi Gari ipo vizuri?

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad