Wakili wa kujitegemea, Fatma Karume, amemtolea povu Spika, Job Ndugai, kuhusiana na wabunge waliovuliwa uanachama na kusema anaendelea kuvunja katiba na kanuni za bunge.
Fatma aliandika ujumbe huo katika ukurasa wake wa twitter akijibu taarifa iliyowekwa na bunge ikionyesha maelezo ya Spika Ndugai kuhusu wabunge wa Chadema waliovuliwa uanachama.
“Job kavunja katiba na anavunja katiba, Job kavunja kanuni za bunge na anaendelea kuzivunja. bahati nzuri hilo bunge pia linavunjwa karibu ili tuanze upya ,” aliandika Fatma
Jana Ndugai ameahidi kuwalinda wabunge waliofukuzwa uanachama wa Chadema akisema hakuna mwenye mamlaka ya kumfukuza mbunge yeyote isipokuwa yeye ambaye aliwaapisha.
Ndugai amesema wabunge wasiwe na hofu yoyote kwani taarifa anazosikia kwenye mitandao ni vikao vya majungu, Amehojoji ni nani huyo anayewafukuza watu na mamlaka hayo anayapata wapi kama bunge halijamtuma.
Jana kamati Kuu ya Chadema imewavua uanachama wabunge wake wanne baada ya kukaidi amri ya kukaa karantini na kuendelea kuhudhuria vikao vya bunge
Job kavunja KATIBA na anavunja KATIBA! Job kavunja Kanuni za Bunge na anaemdelea kuzivunja. Bahati nzuri HILO BUNGE PIA LINAVUNJWA KARIBU ili tuanze UPYA!!!
— fatma karume aka Shangazi (@fatma_karume) May 11, 2020