Hapi Arejesha Gari la Mwalimu Aliyetapeliwa

 
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mkoani Iringa katika kipindi cha kuanzia mwezi Januari hadi Juni, 2020 imeweza kuokoa kiasi cha fedha zaidi ya shiliingi bilioni 1.2.


Kamanda wa TAKUKURU Mkoa wa Iringa, Mweli Kilimali amesema, katika kipindi hicho cha ufuatiliaji wa madeni ya wadaiwa sugu vyama vya akiba na mikopo (SACCOS) 67, vilifikiwa na zaidi ya bilioni 1.2 ziliokolewa.

Mbali na fedha hizo pia amesema kuwa katika opresheni ya kuwatafuta wakopeshaji wa mikopo umiza, wamefanikiwa kukamata  gari lenye namba ya usajili T 311 DDF aina ya Nissan Serena iliyokuwa mali ya mwalimu mstaafu Hadija Nassor Mazola aliyekopa kiasi cha Mil 2 mwaka 2017 kutoka kwa mkopeshaji Micheal Wilson Sanga.

Kwa upande, Mkuu wa Mkoa wa Iringa Ally Hapi ameipongeza TAKUKURU kwa kazi nzuri ya kuokoa fedha na mali za wananchi.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad