Hatari ya Kufariki....WHO Yasitisha majaribio ya hydroxychloquine Kama Tiba Ya Corona



Shirika la Afya ulimwenguni WHO, limesema linaahirisha majaribio ya dawa ya hydroxychloroquine kama tiba ya ugonjwa wa COVID-19.

Mkuu wa shirika hilo Tedros Adhanom Ghebreyesus amesema wanachunguza usalama wa dawa hiyo.

Uamuzi huo wa WHO umefikiwa baada ya ripoti ya wanasayansi iliyochapishwa katika jarida maarufu la kitabibu la The Lancet wiki iliyopita, ikisema matumizi wa hydroxychloroquine yalikuwa yakizidisha hatari ya kufa miongoni mwa wagonjwa wa COVID-19, amesema mkuu wa shirika hilo Tedros Adhanom Ghebreyesus katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika kwa njia ya video jana jioni.

Tedros alisema kile kinachofahamika kama 'mshikamano wa majaribio' kinachohusisha mamia ya hospitali ulimwenguni ambazo zimekuwa zikiijaribu dawa hiyo kwa wagonjwa wa virusi vya corona kimeacha majaribio hayo kama hatua ya tahadhari tu. Mkuu wa huduma za dharura katika shirika la WHO Mike Ryan amesisitiza kuwa hakuna matatizo mengine yaliyojitokeza.

Ingawa dawa hiyo awali ilitumiwa kutibu malaumivu ya misuli, baadhi ya watu, rais Donald Trump wa Marekani miongoni mwao, wamekuwa wakiipigia debe kama tiba kwa virusi vya corona, na nchi kadhaa zimekuwa zikiiagiza kwa wingi. Wiki iliyopita, waziri wa afya wa Brazil alishauri matumizi ya dawa hiyo, pamoja na nyingine ya Chloroquine inayotibu malaria, kwa ajili ya wagonjwa wa COVID-19.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad