Mchekeshaji Idris Sultan anashikiliwa na jeshi la polisi toka siku ya jana bila taarifa rasmi ya sababu ya kushikiliwa na jeshi hilo huku tetesi zikidai kwamba ni makosa ya mtandaoni.
Hii ni mara ya tatu kwa hivi karibuni kwa mchekeshaji huyo kushikiliwa na jeshi la polisi kutokana na makosa mbalimbali. Kosa la kwanza ambalo alishikiliwa na kuhojiwa ni kuhusu picha za Rais Magufuli mwishoni mwa kwaka 2019.
Mara ya pili ni mapema mwaka huu ambapo alipandishwa mahakamani yeye pamoja na baadhi ya viongozi wenzake kutokana na kuweka maudhui mtandaoni bila kuwa na kibali.
Na siku ya jana mchekeshaji huyo anadaiwa kushikiliwa na jeshi la polisi kwa makosa ya mtandao kitu ambacho bado hakijathibitishwa. Mpaka sasa hivi bado anashikiliwa na jeshi la polisi huku mwanasheria wake wakiendelea kufuatilia suala la dhamana.
Je wewe una maoni gani juu ya Idris Sultan na kipi kipo nyuma yake?