Je, Kuna Uhusiano wa Mtu Kufungulia Mziki mkubwa wa Sabufa na Uelewa au Kipato Chake?


Naomba kufahamu hili jambo kutoka kwenu, japo mapovu najua yatakua mengi hapa! Hivi kuna uhusiano wa mtu kufungulia mziki mkubwa wa sabufa na uelewa + kipato alicho nacho?

Nataka kulifahamu hili kwa sababu nilikuwa maeneo fulani ya kijiweni wadau wakidai mara nyingi watu ambao hufungulia miziki mikubwa ya sabufa ni watu ambao wana mambo ya kitoto kitoto (uelewa mdogo) + kipato kidogo cha fedha + kukosa mambo ya maana ya kufanya.

Haswa pale mtu akiwa room kwake au kwenye makazi yake.


Sasa je? Hili lina uhalisia wowote (haswa kwenye jamii zinazotuzunguka?) au lina ukweli wowote!?

Pia wameenda mbali wakidai kuwa huwezi kuta watu wenye mpunga mrefu wana makelele ya redio au mziki mkubwa ....mara nyingi ni silence!

Ila choka mbaya wana mafujo kama yote

Ni kweli!? Karibu.

NAWASILISHA

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Ni kweli kabisa. Hii nime i prove beyond any doubt.
    Kuna watu unakuta hata madirisha kwenye nyumba hawajaweka, bati limeliwa na kutu, lakini akifungulia hiyo sub woofer hatusikilizani.
    mwingine jirani yangu ana kagari kabovu kila siku kanapigwa spana, ila kila akipita ni muziki na makelele yasiyo namsingi.
    kipato na elimu vinachangia sana katika hili, you are very right.
    Regards,

    ReplyDelete
  2. Dah Mwandishi upo sahihi kabisa

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad