Ni hivii, nimekutana na mtu siku za karibuni na kuanzisha urafiki wa kawaida tu. Sasa katika mazungumzo likaja swala la mapenzi na wivu. Mwenzangu anaamini kuwa na wivu sio mapenzi kwa kuwa, wivu ni dalili ya kumnyima mwenzio kupata kile roho inapenda. Kwamba, kwake yeye hata kama ikitokea akaoa, hatomnyima mke wake kutembea na mwanaume mwingine yeyote atayependa. Tena ikibidi atume na video kabisaa ili impe stimu wakati manzi ake analiwa.
Wakuu, je ni kweli wivu ni dalili ya uchoyo? Na kwamba kama unampenda mtu kwa dhati huwezi kuwa mchoyo kwake. Kule uzunguni mume/mke huwa wanapeana nafasi ikitokea mmoja wapo kamtamani mtu mwingine wanakubaliana kuonja. Tuwaeleweje hawa watu? Maana ni binadamu wenzetu.
Nawasilisha hoja kwa majadiliano.
Karibuni
Kule uzunguni Je uliishawahi kufika ukayaona hayo uliyoyaandika au ndiyo hizo za "nimesikia uzunguni kuwa eti..."
ReplyDeleteget yourself something to do...unataka tujadili nini hapa? old witch!
ReplyDeleteTusipende kuiga mambo ambayo hayatupi faida yeyote tuige mambo mazuri tu.Na kama wanatabia hizo ni wao sisi tubaki na tabia zetu na tamaduni zetu.
ReplyDelete