Jeshi La Polisi Dodoma Lakamata Magari 6 Ya Wizi......latangaza Dau La Milioni Moja Kwa Mtu Atakayesaidia Kutoa Taarifa Za Wizi Wa Magari
0
May 15, 2020
Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.
Jeshi la Polisi mkoani Dodoma linayashikilia magari sita yanayodhaniwa kuwa ya wizi .
Akizungumza na Waandishi wa habari leo Mei,14,2020 jijini Dodoma Kamanda wa Polisi mkoani hapa SACP Gilles Muroto amesema mnamo tarehe 10/05/2020 majira ya saa 10 kijiji cha Mbande ,kata ya Sejeli ,wilaya ya Kongwa mkoani Dodoma barabara kuu ya Morogoro –Dodoma , lilikamatwa gari Na.T.936 Toyota Land Cruiser VX Rangi nyeupe ,Chassis Na.HDJ800003615 na Engine Na.1HZ80-0019603.
Kamanda Muroto amebainisha kuwa katika uchunguzi wa awali gari limegundulika kutofautiana na taarifa zilizopo kwenye kadi inayoonesha Chassis Na.HZJ800019603 na Engine Namba 0111948 tofauti kabisa na uhalisia na kutiliwa mashaka kuwa ni mali ya wizi.
Dereva Ramadhan Zaniel Sekiondo [31] mkazi wa Magomeni Mikumi Dar E s Salaam alikuwa akilipeleka mkoani Tabora kwa mtu asiyemfahamu akitokea Dar Es Salaam baada ya kukabidhiwa na mtu asiyemfahamu anayeishi jiji Dar Es Salaam .
Katika tukio la pili Kamanda Muroto amefafanua kuwa mnamo tarehe 11/5/2020 eneo la Area A kata ya Kizota jijini Dodoma yalikamatwa magari mawili yaliyokuwa yamehifadhiwa kwa kufungiwa ndani ya nyumba yasiyo na Namba za usajili yakitumia Namba ya Chassis ambayo ni Toyota HARRIER Chassis Na.MCU310001691,Engine Na.1MZ1589700 na Toyota IST Chassis Na.NCP600209833 Engine Na.2MZ3578179.
Katika uchunguzi wa awali imegundulika kuwa hayana kumbukumbu zozote na yaliingia nchini bila Uhalali huku uchunguzi zaidi ukiendelea kwa kushirikiana na Interpol na mtuhumiwa Omari Chilipachi [29] mkazi wa Sinza DSM anahojiwa na jeshi la Polisi.
Aidha,siku hiyohiyo, Eneo la Area A Kata ya Kizota jijini hapa lilikamatwa gari aina ya Land Rover Discovery lenye namba za usajili wanchi ya Afrika kusini namba SJV576 GP Chassis Na.SALLAAA135A339616 ambazo zinatofautiana na zilizopo katika gari 049053121030305071757 ambalo halipo kwenye mfumo wa usajili wa magari na mtuhumiwa Jamal Swalehe Rasidi [28] mkazi wa Area A anaendelea kuhojiwa na jeshi la polisi.
Katika tukio jingine,Kamanda Muroto amesema mnamo tarehe 12/5/2020 eneo la Nzunguni jijini Dodoma lilikamatwa gari aina ya Toyota Alphard lenye kadi Na.384 DMU lenye Chassis Na. ANH100038956 Engine Na.2AZ1184313 ambapo katika uchunguzi wa awali ulibaniwa kuwa chassis ANH100030547 na Engine ZNZ 0860988 halisi kwenye gari zinatofautiana na lililetwa Dodoma kwa matengenezo kutoka Mbeya na Mtuhuiwa Gofrey Amos Sanga[37] mkazi wa Nzunguni anaendelea kuhojiwa.
Mnamo tarehe 13/5/2020 stand ya Daladala Sabasaba jijini Dodoma lilikamatwa gari Na.T.589 BAD aina ya Toyota Hiace yenye Chassis LH1741000724,Engine 5L5091996 na baada ya ukaguzi wa awali liligundulika kutofautiana na namba halisi ambazo ni chassis LH12330013812 na Engine 3L4538966.
Hata hivyo kamanda Muroto amesema wilayani Kondoa na Dodoma katika mwendelezo wa msako wa wezi wa pikipiki walikamatwa watuhumiwa wawili wa wizi wa pikipiki .
Pia,Kamanda Muroto amebainisha kuwa mnamo tarehe 13/5/2020 eneo la Medeli kata ya Tabuka Reli jijini Dodoma alikamatwa Shaban Nyamhanga Wisandala [32] mkazi wa Medeli akijifanya afisa usalama wa taifa na kuwatapeli watu pamoja na kuwafanyia vitishio.
Jeshi la Polisi mkoani Dodoma limetoa dau la Tsh.milioni moja kwa mtu atakayesaidia kutoa taarifa ya wizi wa magari
Tags