Jeshi la Polisi Limepiga Marufuku Mikusanyiko ya watu Hasa Sherehe za Eid el Fitri
0
May 22, 2020
Jeshi la polisi limesema kuwa sikukuu ya Eid el Fitri itasherehekewa huku dunia ikiwa imekumbwa na ugonjwa wa Corona, hivyo wananchi wanatakiwa kuchukua tahadhari.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo na Msemji wa jeshi la polisi, David Misime imeeleza kuwa jeshi polisi linatoa wito na msisitizo mkubwa kwa Watanzania kusheherekea huku wakizingatia kimamilifu maelekezo yaliyotolewa na yanayoendelea kutolewa na viongozi wakuu na wataalamu wa afya ya namna ya kujikinga na Corona.
“Tuna uhakika kila mmoja kuzingatia maelekezo hayo kuanzia ngazi ya familia mafanikio makubwa ambayo tumeanza kuyapata katika kukabiliana na ugonjwa huu nchini kwetu ,” amesema.
taarifa hiyo imeeleza kuwa jeshi la polisi halitegemei na halitarajii kupambana na watu kutokana na kukiuka maelekezo ya kujikinga na maambukizi ya Corona.
“Tunategemea kila mmoja kwa nafsi yake kuthamini maisha yake na kufuata maelekezo, hivyo hatutegemei watu kuwa katika mikusanyika isiyo ya lazima kama viongozi na wataalamu walivyoelekeza na hata viongozi wa dini watakavyowaelekeza,”
Aidha, wakati wa sherehe hizo jeshi la polisi limejipanga kikamilifu kuhakikisha hali ya ulinzi na usalama inakuwa ni ya uhakika na kwamba waumini wa dini ya Kiislamu na Watanzania wote wanasherehekea katika mazingira ya amani na utulivu.
Tags