Kabudi Asema Rais Hakuhudhuria Mikutano ya viongozi wa EAC, Sadc Sababu Haikuwa Rasmi


.

Waziri wa mambo ya nje ya Tanzania Profesa Palamagamba Kabudi amefungukwa kwanini Tanzania haikushiriki mkutano wa jumuiya za kikanda iliyofanyika hivi karibuni kujadili mambo ya corona akisema haikuwa rasmi na mingine ilikuwa haiihusu nchi.

“Tusiruhusu maadui zetu kutaka kuitingisha Jumuiya ya Afrika Mashariki….wana yaoo…na sisi tusiwe sehemu yao… mkutano ule ulikuwa ni mkutano wa korido ya kaskazini…” – Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Palamagamba Kabudi.

Kabudi amesema mkutano uliofanyika wa nchi nne ni wa ushorobo wa Kaskazini na Tanzania ilitaarifiwa  na si mara ya kwanza tangu zamani wamekuwa wakifanya hivyo na Tanzania haioni sababu ya kushiriki mkutano usio wake “Ule haukuwa mkutano wa EAC”.

“Rais Ramaphosa hakuita mkutano wa Sadc kwani mkutano wa Sadc unaitwa na Mwenyekiti kwa kushirikiana na Katibu wake ndiyo maana nchi nyingi hazikushiriki na Ramaphosa alisema mkutano wa Sadc haukuitishwa sababu ya Logistics ni kweli”
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad