Kauli ya Max Melo Kwa Wanao Nunua Simu Zilizotumika 'Used' ...."Huenda Simu Hiyo Ilishawahi Kufanyia Uhalifu"
0
May 30, 2020
Mkurugenzi wa JamiiForums na Mtaalam wa Mawasiliano ya Teknolojia, Mexence Melo, amewaomba Watanzania kuepuka kununua simu zilizotumika 'Used' kutoka katika mataifa mbalimbali na hata ndani ya nchi kwa kuwa wanakuwa hawajui historia ya mtumiaji wa hiyo simu.
Melo ameyabainisha hayo leo Mei 29, 2020, kwenye kipindi cha SupaBreakfast ya East Africa Radio, na kuongeza kuwa mtu anaweza kununua simu ambayo ilitumika kwenye uhalifu na hata kwenye mitandao mikubwa ya kigaidi na hivyo endapo simu hiyo itaanzwa kuchunguzwa, basi atakayekamatwa nayo ndiye atakayehusishwa na matukio hayo moja kwa moja.
"Kununua simu iliyotumika si vibaya sana, kama uko tayari kuyachukua yale yote yaliyoambatana na hiyo simu, maana hiyo simu unakuwa nayo karibu kuliko hata mpenzi wako au mtu wako wa karibu, kwahiyo unakuwa umezikubali athari zote zitakazotokea, lakini epuka kununua simu zilizotumika, kwa sababu inakuwa ina historia ambayo hauijui, huenda mwenye hiyo simu alishawahi kuifanyia uhalifu" amesema Melo.
Aidha Melo ameshauri umuhimu wa kila mtu kuwepa nywira 'Password' ambayo siyo rahisi mtu kuipatia na isiwe ile ya mwaka wako wa kuzaliwa
Tags