Kisa Mbuzi, Papai na Oil Chafu...Bosi wa Maabara TAIFA Atumbuliwa


Kufuatia hotuba ya Rais Magufuli jana ambayo ilitaja changamoto za utendaji wa maabara ya Taifa ya Afya ya Jamii, Waziri wa Afya Ummy Mwalimu @ummymwalimu amemuelekeza Katibu Mkuu(Afya) kuwasimamisha kazi Mkurugenzi wa Maabara hiyo Dkt.Nyambura Moremi na Meneja udhibiti wa ubora Jacob Lusekelo kupisha uchunguzi.

Waziri Ummy ameunda Kamati ya Wataalam 10 wabobezi kwa ajili ya kuchunguza mwenendo wa Maabara hiyo ya Taifa ya Afya ya Jamii ikiwemo mfumo wa ukusanyaji na upimaji wa sampuli za Covid-19, kamati itaongozwa na Prof. Lyamuya kutoka MUHAS na itawasilisha taarifa kwa Waziri Ummy kabla ya May 13,2020.

Rais Magufuli jana alizitaja changamoto kadhaa zilizopo kwenye Maabara ya Taifa ikiwemo Maabara hiyo kutoa majibu yaliyoonesha mbuzi na papai kukutwa na corona.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad