Korea Kusini na Kaskazini zashambuliana kwa bunduki


Serikali ya Korea Kusini imesema leo wanajeshi wake wamefyetuliana risasi na wanajeshi wa Korea Kaskazini katika eneo lisilo na shughuli za kijeshi linalozitenganisha Korea mbili.

Taarifa ya mkuu wa majeshi wa Korea Kusini imesema kituo kimoja cha walinzi kilishambuliwa kwa risasi kadhaa kutoka upande wa kaskazini, lakini hakuna aliyejeruhiwa.

Afisa huyo wa jeshi amesema jeshi la Korea Kusini lilifyetua risasi kujibu shambulizi hilo na kutoa onyo kwa wanajeshi wa upande wa kaskazini.

Makabiliano hayo ya nadra yametokea siku moja tangu vyombo vya habari vya Korea Kaskazini kuripoti kuwa kiongozi wake Kim Jong Un ameonekana hadharani kwa mara ya kwanza katika kipindi cha karibu wiki tatu.

Kutoonekana kwa Kim kulizusha uvumi kuhusu hali yake ya afya na wasiwasi juu ya hatma ya taifa hilo linalokabiliwa na mbinyo wa kutengwa kimataifa kutokana na mpango wake tata wa silaha za nyuklia.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad