Kufuatia Kauli za Rais Magufuli, Waziri Ummy Achukua Hatua Nzito Maabara inayopima Covid-19



Ujumbe wa Waziri Ummy Mwalimu kwa Rais Magufuli – Millardayo.com

Waziri wa afya Ummy Mwalimu amewasimamisha kazi Mkurugenzi wa maabara ya taifa ya afya ya jamii Dk Nyambura Moremi na Meneja udhibiti ubora wa Jacob Lusekelo ili kupisha uchunguzi kufuatia kauli ya Rais John Magufuli jana.

Pamoja na hatua hiyo Waziri Ummy ameunda kamati ya watalaam 9 ikiongozwa na Profesa Eligius Lyamuya wa Chuo kikuu cha Muhas ili kufanya uchunguzi wa mwenendo wa baabara ya taifa ya jamii ikiwemo mfumo mzima wa ukusanyaji wa sampuli za ugonjwa wa corona (Covid-19).

Ummy amesema kamati hiyo imeanza kazi mara moja (kuanzia leo Mei4, 2020) na itatakiwa kuwasilisha taarifa yao kwa Waziri kabla ya mei 13, hata hivyo amesema shughuli za upimaji katika maabara hiyo zitaendelea kama kawaida.


Itakumbukwa kuwa jana katika hotuba yake Rais John Magufuli baada ya kumuapisha waziri Mpya wa katiba na sheria alisema kuna warakini katika vipimo vya Covid-19 nchini akisema ofisi yake ilipeleka sampuli ya vitu mbalimbali ikiwemo papai, fenesi, oili, mbuzi na kondoo babdo vimo vikatoa majibu na kati ya vitu hivyo kuna vilivyokutwa na ugonjwa wa corona.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad