"Sikulazimishwa kuzaa...Usizae Kama Haujajipanga" Hamisa Mobetto







Licha ya kwamba Star wa kike Hamisa Mobetto amezaa Watoto wawili nje ya ndoa, bado ana imani kupitia Ubalozi alioupata kwenye ‘kampeni ya sitetereki’ ataweza kuwasaidia wengine wenye mitazamo tofauti kuhusu afya ya uzazi.

“Sikulazimishwa kuzaa nilikuwa nipo tayari na nilijipanga ndio maana nipo hapa kuwaambia kuwa sio rahisi, usizae kama hauko tayari au haujajipanga, tamaduni zetu tumezoea matunzo anatoa Baba"-Hamisa

Mobetto ametoa kauli hiyo leo wakati akipewa Ubalozi wa ‘kampeni ya sitetereki’ inayosimamiwa na kampuni ya Smart Generation inayoongozwa na Nikk wa Pili na Mtangazaji Cza wa Clouds FM.

Hamisa anakua Balozi wa Pili baada ya Msanii Nandy kutambulishwa kama Balozi hivi karibuni.
OPEN IN BROWSER

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Mola azidi kukufungulia kila la kheri, Hamisaaaa

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad