Tundu Lissu Aibuka na Lijulikali "Hakusema Ukweli Wote..Sasa Amepanda bei"
2
May 21, 2020
Anaandika Tundu Lissu
Hili la CHADEMA na tuhuma dhidi ya Mwenyekiti Mbowe jibu lake hili hapa:
Haya malalamiko sio ya jana na sio ya juzi; na sio ya mwaka jana wala mwaka juzi. Tangu nimeingia CHADEMA mwaka 2004, kila kiongozi ambaye ameondoka CHADEMA na kujiunga na CCM amehalalisha kuondoka kwake kwa kutoa tuhuma za matumizi mabaya ya fedha za chama.
Sio Lijualikali na Silinde na Mwambe wa leo tu. Kila kiongozi - kuanzia marehemu Amani Walid Kabourou na Chacha Wangwe na kuendelea - amelalamikia matumizi mabaya ya fedha za chama pale anapoondoka kwenye Chama. Na mgomvi wao wa miaka yote ni Mwenyekiti Mbowe, sio Dr Slaa au Dr Mashinji waliokuwa Makatibu Wakuu wa Chama wa hivi karibuni.
Cha ajabu ni kwamba hakuna hata mmoja ambaye amewahi kuthibitisha madai yao haya. Ajabu nyingine ni kwamba wanatoa tuhuma wakati wa kuondoka kwenye Chama tu. Wakati wakiwa ndani hakuna shida.
Fedha za chama cha siasa ni fedha za umma; ndio maana hukaguliwa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kila mwaka. Ndio maana hukaguliwa pia na wahasibu huru na mahesabu hayo hupelekwa kwa Msajili wa Vyama vya Siasa kwa ukaguzi zaidi.
Ubadhirifu au matumizi mabaya ya fedha hizo ni kosa la jinai kwa mujibu wa sheria za nchi yetu. Mwenye kutenda makosa hayo alipaswa na anapaswa kuchukuliwa hatua za kijinai kwa mujibu wa sheria za nchi yetu.
Sasa kama Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu na Msajili wa Vyama vya Siasa na wahasibu wa kujitegemea hawajawahi kuona huo ubadhirifu au matumizi mabaya fedha, hawa wanaolalamikia jambo hili, hasa wanapoelezea sababu za kuondoka kwenye Chama na kujiunga na CCM wanawezaje kuwa taken seriously???
Kwa nini hamuwaulizi hata uthibitisho wa tuhuma hizo, kama sio kujaribu kuficha sababu halisi za kukimbia kwao kwenye Chama???
Kwa jinsi ambavyo mamlaka za Serikali ya Magufuli na ya Kikwete kabla yake ambavyo zimekuwa zinatuchukia, kama kweli kungekuwa na ubadhirifu tunaotukanwa nao miaka yote hii, tungeshafungwa wote zamani. Huyu Mbowe si angeshaozea gerezani???
Badala yake, tumekuwa Chama Kikuu cha Upinzani katika nchi yetu licha ya matusi yote haya na licha ya uonevu mkubwa ambao tumeendelea kufanyiwa. Tunasonga mbele.
Kuhusu Wabunge kuchangishwa michango mbali mbali. Tofauti na CCM ambayo huchotewa pesa za serikali na za wafanya biashara wanaohitaji tender au leseni mbali mbali, CHADEMA imejengwa kwa michango ya wanachama, hasa Wabunge.
Wabunge wa CHADEMA miaka yote wamechangia fedha, magari na muda wao kwa ajili ya shughuli za Chama. Ndio maana tumeweza kupata Wabunge, madiwani na Wenyeviti wa Vijiji na Mitaa wengi. Hawa akina Lijualikali na wenzake wanaolalamika sasa hivi, walipatikana kutokana na michango ya Wabunge waliokuwapo kabla yao.
Nimemsikia akidai kwamba alichangiwa na wananchi wake tu. Ni mwongo. Mimi mwenyewe nimemchangia kwa fedha, mali na muda wangu. Nimekwenda kumfanyia kampeni za uchaguzi wa Diwani wa Kata ya Ifakara mwaka '13 kwa gharama zangu mwenyewe.
Nimemsaidia kesi ya Ubunge wakati hawa maswahiba zake wa sasa walipojaribu kumvua Ubunge wake kihuni. Nimemsikia akilia Bungeni kwamba alifungwa jela miezi sita kwa uonevu kwa ajili ya CHADEMA.
Hakusema ukweli wote. Hakusema nani aliyemhangaikia Mahakama Kuu kwenye rufaa mpaka akatoka gerezani. Mimi sio tu nilimtetea mahakamani; nilienda kumwona gerezani Ukonga na kumfariji. Baba yake mzazi ni shahidi yangu.
Hakusema kama alisaidiwa na chama au na sisi wanachama wenzake. Hawezi kusema amewahi kutulipa au kuwalipa hao waliomsaidia kiasi gani cha pesa. Hakusema na hatasema kwa sababu anajua jinsi ambavyo Chama chake na wanachama wenzake walivyombeba.
Sasa amepanda bei anaomba CCM wampe kazi. Wale wale waliomfunga na kumnyanyasa na kumdhalilisha mara nyingi, sasa ndio maswahiba zake. Sisi tuliomsaidia kwenye shida yake hatuna maana tena. Hamna shida. Tunasonga mbele.
Nilichokisema kuhusu Lijualikali linawahusu Wills Lwakatare na Cecil Mwambe na David Silinde. Wamebebwa na chama na viongozi na wanachama. Sasa Chama hakiwababaishi tena.
Siwezi kuwaambia wakumbuke walikotoka, maana hawatakumbuka. Nawasihi wajiulize walikoishia waunga juhudi za Rais wengine wote wa miaka ya nyuma.
Tags
Kweli wee Roho yako mbaya, Unata m/kiti
ReplyDeleteAozee jela. Au umeshapata tetesi za mchongo waliofanya kukumaliza?
Binaadamu unacheka nao na unakula nao
Lakini hawa aminiki nasikia ulimpiga
fullstop m/kiti kukutembelea, je ni kweli? nao unaendeleaje na dozi?
Lijualikali ni mmoja wa Wabunge Nyota
ReplyDeleteChadema anae jielewa kama Wenzake a
walioweza Kuhoji na kuchukua uamuzi sahihi inapo bidi, na ndiyo alichofanya kwenda kinyume na uamusi wa Genge la SACCOZ yao.
Hongera kwa kutokubali kupelekeshwa akina heche na kundi lako amkeni hata tundu ameanza kushtukia mchongo ulio
mfikisha hapo alipo..ngoma ina anza
kuwa tamu, Sindimba..!!! kwachu kwachu