Madam Rita wa BSS Aanza Kutekeleza Agizo la Serikali la Kumlipa Mshindi wa BSS Milion 50


Serikali imeipongeza Kampuni ya Benchmark kwa kutekeleza maelekezo yake kuhusu malipo ya Mshindi wa BSS 2019 Meshack Fukuta kwa kumlipa sehemu ya fedha anazodai na kuahidi kumalizia kiasi kilichobaki.

Taarifa iliyotolewa na Naibu Waziri wa Sanaa, Juliana Shonza kupitia ukurasa wake wa lnstagram @Juliana_Shonza, imesema.

Naipongeza Kampuni ya Benchmark kwa kutekeleza maelekezo ya Serikali kuhusu malipo ya mshindi wa BSS 2019 Bw. Meshack.

Jana tarehe 15/05/2020 Mkurugenzi wa Benchmark Madam Rita chini ya usimamizi wa Basata amekabidhi kiasi cha Shilingi milioni tano ikiwa ni sehemu ya fedha ya zawadi kwa Bw. Meshack,hata hivyo kutokana na changamoto mbalimbali za kifedha walizokumbana nazo kwenye msimu uliopita, Benchmark wameomba kuongezewa muda kidogo na wameahidi kumalizia kiasi kilichobaki ndani ya muda mfupi ujao.

Serikali imeridhia maombi hayo na nimatumaini yetu kuwa Benchmark watafanya kama walivyoahidi.

Aidha ili kuepusha kujitokeza kwa mazingira kama haya katika mashindano yajayo, Serikali itahakikisha utaratibu wa waandaaji wa mashindano kukabidhi zawadi husika kwa Basata kabla ya fainali ya mashindano unatekelezwa.

Vilevile nitoe wito kwa Benchmark na wadau wengine wanaoendesha mashindano mbalimbali ya vipaji kuzingatia kuweka zawadi wanazoweza kuzimudu kulingana na maandalizi yao ili kuepusha usumbufu usio wa lazima.

Tuwekeze nguvu kubwa katika kuhakikisha mashindano haya yanatumika kama majukwaa ya kuibua vipaji na kupata jukwaa la kuonyesha vipaji vyao na sio jukwaa la kupata fedha nyingi,japo sio mbaya kama uwezo utaruhusu.

Hata hivyo serikali inapongeza jitihada hizi za uongozi wa Benchmark na tunaahidi kuendelea kushirikiana na Madam Rita katika kuibua , kukuza na kuendeleza vipaji vya muziki hapa nchini kupitia jukwaa la Bongo Star Search.

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Kichwa Cha Habari na Maudhui yameendana Sawa.

    HONGERA WIZARA NA BARAZA.

    MUENXELEE KUHAKIKISHA HAKI YA HAWA VIJANA INAWAFIKIA KUPITIA NYINYI VYOMBO HUSIKA.

    HONGERA MAMA SHONZA NA TIMU YAKO NA BARAZA PIA KWA UFATILIAJI NA MIKAKATI YA HAPO BAADAE KATIKA UBORESHAJI.. NA KAYUMBA PIA ANA HAKI YAKE YA MSINGI MS RITHA ANALIELEWA HILO

    ReplyDelete
  2. Hongerwni Wadau wote WA Tasnia.
    Tunachoomba muwe WA kweli na Waadilifu na mumuogope MUNGU kwa Nia njema.

    Ubabaishaji na Utapeli muuweke kando.

    Hakikisheni Dhulma mnaipiga Vita. A Kayumba na Meshack wanapata haki zao Japo Kayumba hakwenda KATIKA Vyombo vya Habari. UKWELI UJAJULIKANA NA WA HUSIKA WANALIELEWA HILO

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad