Mahakama ya Kisutu yamkuta Mdee na kesi ya kujibu




MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imesema baada ya kupitia ushahidi uliowasilishwa mahakamani hapo na upande wa Jamuhuri, imejitosheleza kwamba Mbunge wa Kawe, Halima Mdee ana kesi ya kujibu. 

Uamuzi huo ulitolewa jana mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba baada ya kupitia hoja za pande zote mbili. 

Akisoma uamuzi huo jana, Hakimu Simba alisema mshtakiwa anakabiliwa na shtaka moja la kutumia lugha ya matusi dhidi ya Rais John Magufuli. 

Inadaiwa Julai 3 mwaka 2017 maneno ya Makao Makuu ya Chadema, Mdee alitumia lugha ya matusi dhidi ya Rais Magufuli akisema ‘anaongea hovyo hovyo anatakiwa afungwe breki’. 

Alisema Februari 20 mwaka huu upande wa Jamhuri katika kesi hiyo ya uchochezi walifunga ushahidi wakiwa na mashahidi watatu. 

Hakimu Simba alisema upande wa utetezi waliwasilisha hoja wakiishawishi mahakama imuone mshtakiwa kwamba hana kesi ya kujibu. 

“Mahakama imepitia kwa makini ushahidi, hoja zilizowasilishwa na msimamo wa kisheria nimejitosheleza kwamba mshtakiwa ana kesi ya kujibu,”alisema. 

 Baada ya kusema hayo Hakimu Simba alitaka kujua mshtakiwa atajitetea kwa mfumo upi na atakuw na mashahidi wangapi kama ambavyo sheria inataka. 

Akijibu Wakili wa utetezi, Hekima Mwasipo alisema mtuhumiwa atajitetea kwa kiapo na atakuwa na mashahidi watano. 

Mahakama iliahirisha kesi hiyo hadi Juni 25 na 26 kwa ajili ya mshtakiwa kuanza kujitetea. 

Katika kesi hiyo, inadaiwa Julai 3,2017 katika Makao Makuu ya Ofisi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) mtaa wa Ufipa Wilaya ya Kinondoni, Mdee alitamka maneno dhidi ya Rais John Magufuli kuwa “anaongea hovyohovyo , anatakiwa afungwe breki” na kitendo ambacho kingeweza kusababisha uvunjifu wa amani. 

Mdee alifikishwa mahakamani hapo Julai 10, 2017 na yupo nje kwa dhamana. 


Tags

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Kuna usemi ASIYE SIKIA LA MKUU...
    Na waheng walisema, ASIYE FUNDWA NA MAMAE....

    MUFASA Atakufunda. Walimwengu yetu...!

    ReplyDelete
  2. Kwa Taarifa yenu Bunge litavunjwa siku
    za Karibuni, ndiyo itakuwa ukomo wenu
    kuwawakilisha walio kuchagueni.

    Hii maana yake ni nini.?

    Una Funga kujihusiha umbwabjikaji
    wa kubeza Serikali iliyo Madarakani.
    na msijifikirie kwamba mtahamia twitter na sinapu chati au fesibuku
    kuendeleza Utovu wa Nidhamu na Ukosefu
    wa Heshima na kuto tii Mamlaka.

    Fikisha huu ujumbe hapo Saccozini
    na uwataarifu wana saccos wote akiwepo
    mnya Kiti na Genge lake kuwa leseni ya
    Kubeza ina expire katika wiki 3 zijazo

    Ngoma kwenu kuufyata.

    TCRA Na Mamlaka zote ikiwemo Uhamiaji
    (Mama Makekele / Ali Mtanda) kuhakikisha hati nyekundu zinarudishwa
    haraka iwezekanavyo to avoid misuse.

    Amani na Utulivu wa Nchi yetu ni Jukumu letu Wazalendo.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad