Mahakama yasema Mbunge Mwenye KESI ya Uhujumu Uchumi, Kukutwa na Silaha Apewe Dhamana




Mahakama kuu ya Tanzania Kanda ya Shinyanga, imetoa maamuzi kuwa mbunge wa CCM Jimbo la Kishapu Suleiman Nchambi, anashitakiwa kwa makosa 12 ya uhujumu uchumi, ana haki ya kupewa dhamana kwa masharti.

Jaji wa Mahakama kuu ya Tanzania Kanda ya Shinyanga Phocus Mkeha, ambaye alikuwa akisikiliza maombi ya dhamana hayo amesema masharti ya dhamana hiyo kusaini bondi ya Shilingi Milioni 50, na mdhamini wake bondi ya Milioni 10, pamoja na kushikiliwa hati yake ya kusafiria.

Hata hivyo maamuzi ya utoaji wa dhamana hiyo ameyarudisha katika mahakama ya wilaya ya Shinyanga mahali kesi yake ya msingi ilipoanzia, ambapo wao ndio watasimamia masharti hayo.
Kesi ya Mbunge huyo wa Kishapu kwa mara ya kwanza ilisomwa Mei 8 mwaka huu katika Mahakama ya wilaya ya Shinyanga ambapo alisomewa mashitaka 12 ya uhujumu uchumi, kumiliki Silaha (Bunduki), na risasi kinyume na sheria.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad