Makonda ataka mkandarasi kukabidhi stendi ya Mbezi kwa wakati
0
May 26, 2020
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda ametoa agizo kwa mkandarasi wa Ujenzi wa Stendi mpya ya mabasi ya mikoani na nje ya nchi ya Mbezi Louis ambayo ujenzi wake kwa sasa umefikia 70% kuhakikisha Ujenzi huo unakamilika na kukabidhiwa kwa wakati.
RC Makonda amesema ujenzi wa Stendi hiyo unagharimu kiasi cha shilingi bilioni 50.9 na itakuwa na uwezo wa kuegesha mabasi makubwa 700 na magari madogo yasiyopungua 300 ambapo ndani yake kutakuwa na jengo la abiria, jengo la utawala, “Shopping mall’s”, Hoteli, Hosteli kituo cha polisi, matawi ya bank, Migahawa na eneo la wafanyabiashara wa chakula.
Aidha RC Makonda ameelekeza Manispaa ya Ubungo kuhakikusha ujenzi wa Hospitali ya wilaya ya Ubungo unaanza kabla ya mwezi June na Mkandarasi kuhakikisha ujenzi unakamilika kabla ya mwezi September mwaka huu kwakuwa tayari Rais Dkt. Magufuli aliagiza kujengwa kwa Hospital hiyo lakini cha kushangaza baadhi ya wizara zimekuwa zikipiga danadana kutoa fedha hizo.
Pamoja na hayo RC Makonda ametembelea Ujenzi wa Jengo la manispaa ya Ubungo linalogharimu kiasi cha bilioni 6 ambalo ujenzi wake umefikia 65% na kuwataka TBA kuhakikisha Jengo linaanza kutoa huduma kabla ya mwezi August mwaka huu kwakuwa wamekuwa wakisuasua licha ya kuongezewa muda.
Tags