Makonda Awataka Wananchi Dar Kufanya Shangwe Kushangilia Kuishinda Corona “Piga Kelele Kadri Uwezavyo”


Paul Makonda asaka busara za wazee Dar - MwananchiMkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda amewasihi wafanyabiashara na wananchi wa mkoa huo kuhakikisha wanaanza kufungua biashara zao na kuchapa kazi ili kujenga uchumi wa nchi

Akizungumza leo alipofanya ziara ya kwenye sehemu linapojengwa daraja la Salender jijini humo Makonda amesema hata walioenda mikoni warudi Dar kufanya kazi

“Naomba wenye hoteli wenye mabar turudi kifanyq kazi ilimradi unajua kunawa unajua kunakaa umbali na mwenzio ”

“Mheshimiwa Rais ametoa siku tatu za shukrani kwa watanzania wote lakini mimi niongezee tu ikifika jumapili kila mtu afanye kila aina ya fujo anayoijua kama una disco yako fungua kama unataka kwenda baharini kuogelea sawa tu mimo nimekuruhusu hiyo ni sehemu ya kuonyesha furaha yetu kwa Mungu wetu aliyetishindia” ameongeza

Kauli ya Makonda inakuja iliwa ni siku kadhaa tangu Rais Magufuli atangaze kupungua kwa wagonjwa wa covid Nchini

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad