Mambo ya Wanaume Ambayo Huwakera Wanawake Wengi Kwenye Mahusiano ya Kimapenzi

Mambo ya Wanaume Ambayo Huwakera Wanawake Wengi Kwenye Mahusiano ya Kimapenzi
Hakuna mtu anaependezwa na mpenzi anaeboa. Na kwa mioyo yetu ya kiume hakuna sehemu inayotuumiza na kutuacha tumejawa maswali mengi na paniki kede kede kama pale mambo yanapokuwa hayaendi vizuri kitandani.

Kiumeni.com kama jadi yetu ya kukufanya wewe uwe mwanaume bora zaidi, tumekuandalia mambo saba ambayo yanasababisha hali hii itokee na kumfanya mwenza wako aboreke kitandani na kuishia kutoa visingizio vingine visivyokuwa na maana sababu anaona aibu kukwambia. Visome kwa umakini na uvielewe kama unataka wawe wanarudi na kutaka utamu zaidi.

Unaomba ruhusa
Kama ukiwa unauhusiano wa muda mrefu na mwanamke na umeshaelewa lugha yake ya mwili na hisia zake, hakuna kinachomuondoa kwenye hali ya kihisia kama kuombwa ruhusa ya kiofisi kuendelea na jambo hasa juu ya yale mambo yetu mazuri, hauhitaji karatasi ya mahakama ya ruhusa kuendelea kumpa vishawishi na kumtekenya. Mpenzi mzuri ni yule anaejua kumpa vishawishi na kumfanya asisimke kwa akshi hata kama akili haikua katika hayo mawazo bila ya kukata ushuru wa kuuliza uliza kiasi cha kumuhalibia hisia nzuri zilizokuwa zinaanza kumuingia, vitu vyepesi kama macho mazito ya mahaba au miguso flani ya kumpa akshi ni njia nzuri ya kumuandaa.

Unatabilika
Kama mmekuwa pamoja kwa muda mrefu, hii ndio litakuwa tatizo kubwa maana sababu ya kwanini mara ya kwanza mapenzi yalikuwa matamu kitandani kati yako na yeye ni kwa sababu ulikua hujui nini cha kutarajia. Kama ukiwa unataka kurudisha khali kama awali inakupasa ubadilishe ratiba na ufanyaji wa mambo ili kuleta hali flani ya upya katika uhusiano wenu.

Usiogope kujaribu vitu vipya ambavyo wote kwa pamoja mnaweza kuvipenda, usiache ikafikia hali kiasi akawa anajua mpaka ni kitu gani utachokwenda kinachofatia unachokwenda kukufanya, kwa mfano kama huwa unatumia dakika 5 ukimtaalisha kimapenzi, siku nyingine jaribu kabadilika na kutumia dakika 20 huku ukimsisimua kwa maneno matamu na kumpandisha ashiki kwa kumpapasa kivingine tofauti na unavyopendelea kufanya. Atashangaa mababidiliko na kabla hajajua mtakua nchi za mbali mkitalii.

Mapenzi ya kukurupuka
Mwanamke wako sio punda wa kupandwa bila matayarisho, hajawa doli la kuchezea. Wanawake wote hupendwa kutayarishwa na kupewa mapenzi ya huba yenye hisia, sio mapenzi ya kikurya "Mama Robhii, raraa ni kurariie!". Sio kwa staili hii jamaa, jaribu kuwa mvumbuzi wa mambo, ongeza viungo mtoto wa watu alegee na kusisimka kwa huba na mahaba, usiwe na haraka maana tayari yupo kitandani, mmenye kama ndizi kidogo huku unakula taratibu, kidogo tena huku ukiyaachanisha maganda taratibu na kwa staili ndo unakula tena, we ni mpenzi wake na sio mbakajia, mfanye akuone kama malaika ulioshushwa toka mbinguni kwa kazi moja ya kumpenda na kumpa raha duniani.

Usipojiongeza kwenye mambo mazuri ya kitandani, mwingine mjuzi zaidi yako atakupokonya tonge mdomoni.

Haujiongezi inavyopaswa
Japo wanawake wengi huwa ni rahisi kukubaliana na staili ya mapenzi kutokana na wenza wao, ila iwapo kama unatumia staili hio hio kila mkikutana na hamna vionjo vyovyote vinavyobadilika lazima mwenza wako achoke na kuboleka na utendaji wako wa kazi. Kwahio kama ukitaka asikuchoke inabidi ujiungeze na ufanye mabadiliko ya hapa na pale.

Ndio, umepatishia sahihi lazima ubadilike kimahaba, na sio kitandani peke yake hata nje ya hapo, mnongoneze wakati mnapata chai ni nini utamfanyia giza likiingia, au mtumie meseji tata za jinsi unavyowaza na kutamani giza liingie uwe mikononi mwake, mtoe kwenye mtoko na mpe malavidavyi ya kutosha na utamuacha anawaza umetokea sayari ipi.

Ukifanya kubadilika kila muda utafanya na yeye pia abadilike na kukuonyesha utundu wake wa kike ulipo.

Hautumii maneno au unayatumia kupitiliza
Kutumia sana maneno flani matata kumnongoneza masikioni humfanya mwanamke apandishe mrukhani kwa fujo, ila usitumie maneno yaleyale maana kurudia rudia maneno huyaondolea maana husika na kuyafanya butu. Jaribu kuyatumia katika wakati muafaka na mudi iliyosahihi na fanya uchaguzi mzuri wa maneno matamu yanayoongeza akshi za kimahaba.

Ukimwambia anachokufanyia kinakuuwa maini kwa sauti nzuri ya besi iliyolegea kwa kumnongoneza au ukimwambia ametoka bomba na ukafatiwa na maneno elekezi ya kile ambacho unataka umfanyie kitabadilisha kabisa hali ya kuboreka kwa msichana wako akiwa kitandani na wewe.

Fanya majaribio
Kama upo na mwanamke kwa muda mrefu na unataka mambo chumbani yanoge, unapaswa kubadilisha mikao, jaribu mikao mingine ya kimapenzi, zungumzeni na mwambiane anapendelea nini na angependa kujaribu kipi, mawasiliano ni nguzo kubwa inayoweza kubadilisha mazingira na kufanya staili anayoitamani.

Kumbuka kinyume cha maboreko ni mafurahisho, ukitaka kufurahi jaribu kitu kipya ambacho hujawahi fanya au fanya unachokipenda ila kwa mguso tofauti na fikra mpya.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad