Marekani imewawekea marufuku ya usafiri raia wa kigeni ambao wamekuwa Brazil katika kipindi cha siku 14 zilizopita.
Taifa hilo la Amerika Kusini hivi karibuni limekuwa ngome la pili kuu la maambukizi ya virusi vya corona duniani.
Brazil imethibitisha kuwa zaidi ya watu 360,000 wameambukizwa corona, huku zaidi ya watu 22,000 wakifariki kutokana na baada ya wizara ya Afya ya nchi hiyo kutangaza Jumapili hali ilivyo.
Msemaji wa Ikulu ya Marekani amesema kuwa udhibiti huo wa usafiri utasaidia kuhakikisha hakuna maambukizo mapya yataletwa nchini.
"Hatua ya leo itasaidia kuhakikisha raia wa kigeni ambao wamekuwa Brazil hawatakuwa chanzo cha maambukizi mapya ya corona nchini mwetu," Ilisema taarifa ya Msemaji wa Ikulu ya Marekani Kayleigh McEnany.
Watu wasiokuwa raia wa Marekani na ambao walikuwa Brazil ndani ya muda wa wiki mbili kabla ya kuomba idhini ya kuingia Marekani watazuiliwa kuingia nchini humo. Hatua hiyo haitaathiri biashara kati ya nchi hizo mbili.
Marufuku hiyo ya usafiri haitawajumuisha raia wa Marekani, wanadoa, wazazi, walezi halali, au mto wa raia wa Marekani ama wakaazi wa kudumu, na ndugu walio na umri wa chi ya miaka 21.
"Uwezo wa watu walioambukizwa kupitisha virusi upo juu hasa kutoka kwa wale wanaotaka kuingia Marekani kutoka [Brazil] hali ambayo huenda ikatishia usalama wa mfumo wetu wa usafirishaji na miundombinu na usalama wa kitaifa," ilisema katika amri hiyo ilichapishwa na Ikulu ya Marekani siku ya Jumapili