Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania umedai kuwa hatari ya kupata #COVID19 katika mkoa wa Dar ni kubwa japo hakuna ripoti rasmi za Ugonjwa huo tangu Aprili 29 ila ushahidi unaonesha usambaaji wa #CoronaVirus ni mkubwa.
Ubalozi huo umewashauri Wamarekani waliopo nchini na familia zao kwa ujumla kubaki ndani na kutoka pale yanapohitajika mahitaji muhimu na kuzuia kutembelewa nyumba na watu tofauti tofauti.
Aidha, ubalozi umedai hospitali nyingi za Dar zimezidiwa kwa kipindi cha wiki za karibuni. Ufinyu wa uwezo wa hospitali nyingi Tanzania unaweza kusababisha vifo kutokana na kuchelewa kwa huduma za kitabibu hata kwa wagonjwa wa #COVID19.
Umebainisha kuwa Serikali ya Tanzania imezuia safari zote za Kimataifa za ndege za abiria tangu Aprili 11, hivyo ubalozi umewataa raia wake kubaki ndani ili kujikinga na Corona Virus.