"Mbowe Arudishe Milioni 2 na Wenzake Wote" - Spika


Spika Job Ndugai, amemtaka Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe, kurudisha kiasi cha zaidi ya Shilingi Milioni 2, alizolipwa na Bunge kabla ya kuanza utoro na wabunge wenzake na kwamba wasipofanya hivyo hawataruhusiwa kuingia bungeni, huku pia akiwataka kurudi Bungeni haraka sana


Spika Ndugai ameyabainisha hayo leo Mei 6, 2020, Bungeni Dodoma wakati wa Mkutano wa 19, Kikao cha 22 na kusema kwamba kila mmoja wao ahakikishe fedha zote alizolipwa anazirejesha la sivyo hawatoingia geti la Bunge na hatua kali kuchukuliwa dhidi yao.

"Wabunge hawa ambao ni watoro walipokuwa wanaondoka walilipwa fedha za kuanzia Mei 1 - 17 Jumla ya zaidi Sh Mil 110, nawaagiza kuanzia Freeman Mbowe kurudisha Tsh Mil 2 na elfu 40 na wenzake wote hao, huu ni utoro wa hiari kwa lugha rahisi huu ni wizi na wale wengine wamelipwa Mil 3 warudishe" amesema Spika Ndugai.

Aidha Spika Ndugai ameongeza kuwa  "Nimeshangazwa na kusikitishwa sana na tangazo hilo kwa sababu Mbowe hana mamlaka ya kuitisha utoro wa wiki mbili kwa Wabunge, anajaribu kuwa kama Prefect wa Shule ya Sekondari, japo wameambiana kubaki Dodoma lakini wanazurura nchi nzima, wabunge hao popote walipo warudi bungeni haraka sana kuendelea na kazi zao".
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad