Mchezo wa Kwanza Wapigwa Marekani Bila Mashabiki



Pambano la kwanza la ngumi tangu janga la Corona liingie nchini Marekani limepigwa usiku wa kuamkia leo Mei 10, 2020, ambapo Justin Gaethje amemchapa Tony Ferguson kwa TKO raundi ya 5 na kuibuka bingwa wa UFC interim lightweight.


Pambano hilo limepigwa bila mshabiki kwenye uwanja wa VyStar Veterans Memorial huko Jacksonville, Florida.

Awali pambano hilo lilitakiwa kupigwa 18 April huko Brooklyn lakini likaahirishwa kutokana na Janga la Corona na kupangiwa tarehe ambayo ni usiku wa Mei 10, 2020.

Justin Gaethje mwenye miaka 31, amempiga Tony Ferguson mwenye miaka 36 na sasa ndio bingwa wa UFC Lightweight na atapigana na Khabib Nurmagomedov katika pambano ambalo litapangiwa tarehe baadaye mwaka huu.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad