Naibu waziri wa TAMISEMI Mwita Waitara amesisitiza kuwa hakuna ugomvi wote wote kati ya mkurugenzi wa wilaya ya Ubungo na meya wa halmashauri hiyo Boniface Jacob
Waitara amesema mkurugenzi wa halmashauri alitimiza majukumu yake mara baada ya kupata barua ya chama iliyomfuta uwanachama Meja Jacob
“Imebaki takribani miezi mitano meya kumaliza uongozi wake sasa kama ni hila na chuki si zingefanyika kipindi chote cha nyuma hicho kwa nini mkurugenzi afanye sasa” amesema
“Mkurugenzi ametimiza wajibu wake baada ya kupokea barua ya chama tunafahamu kuna ugomvi wa ndani kati ya meya na mwenyekiti wake wa jimbo ugomvi huo sisi hautuhusu mkurugenzi alichokifanya ni kumvua nyadhifa zote alizozipata kupitia uwanachama wake ambao amevuliwa” ameongeza
Aidha naibu waziri amesema kuwa katibu mkuu wa chama hawezi kumtaka mkurugenzi wa Halmashauri kutimiza wajibu wale
“Mkurugenzi anatimiza wajibu wake kisheria hauwezi kushinikizwa na katibu wa chama cha siasa kufanya majukumu yake na swala la meya kusema anatenda ofisini kwa nguvu ni kama anataka kupambana na dola” amesema
Ikumbukwe kuwa chama vha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) kiliripoti kuwa Meya wa Ubungo Boniface Jacob amevuliwa wadhifa wake kimakosa kutokana na barua ya kughushi ya kuvukiwa uwanachama wa chama hicho
Bonifasi Jakobo, kama una malalamiko, peleka wizara husikka grievance zako na kama huna imani Fugua Jalada Mahakamani.
ReplyDeleteVingievyo kubali hali halisi.