Mfahamu Jaili, Chinja Chinja Aliyevuma Mbeya na Mama yake Aliyekufa na Kufufuka Mara Tatu


Ukifika Mbeya Mjini kuna eneo linaitwa Forest Mpya.

Siku za nyuma eneo hilo lilijulikana tu kama Forest kwa kuwa kulikuwa na msitu mkubwa sana wa miti ya milingoti ambayo Kama huijui ni miti inayozalisha nguzo za umeme na za TTCL.

Huu msitu ndio Jaili aliutumia kuchinja watu ambao alikuwa akiwapiga kwanza na nyundo, Kisha huwapakia kwenye gari na kwenda kuwachinja Forest.

Mama yake Jaili alikuwa ni mchawi sana na alikufa na kufufuka Mara tatu kwenye uhai wake. Na alipokuja Mara ya nne haraka haraka wakaenda kumzika kwenye makaburi ya Nonde.

Mara ya kwanza alifia katika Hospital ya Rufaa Mbeya, enzi hizo ikiitwa Gredi Wani. Alipokufa wakampeleka mortuary, sasa Kuna watu walikuwa na maiti ya ndugu yao kafa kwa ajali, wakati mhudumu anavutavuta mafriji, mama yake Jaili akanyanyuka, na kutembea kwa miguu hadi kwa mwanae mitaa ya Ghana.

Mara ya pili alifia nyumbani kwa mwanae, na akapelekwa mortuary ambako alikaa, na siku walipoenda kumuandaa kwa ajili ya maziko, aliamka na kurudi kuwa hai, watu wakatoka nduki vibaya Sana.

Baada ya siku chache huyu Bibi mwenye mauzauza ambayo USER=98741]Mshana Jr[/USER] hajawahi kuyaona maishani mwake, alifariki Tena, ila Safari hii nimesahau alifufukaje.

Sasa alipokuja kufa Mara ya nne, hawakumchelewesha, Wananzengo fasta wakakimbilia kwenye makaburi ya Nonde, wakachimba kaburi refu sana, ngazi ya zimamoto inazama, wakaandaa na trip ya mawe, jiwe la chuma sio mamoma.

Maiti fasta ikawekwa kwenye jeneza lililotengenezwa kwa mti wa Mkambokambo, ile miti ambayo zamani wakati wa Christmas ilikuwa inauzwa Namanga na Kariakoo Cyprus  tree.

Fasta wakaitwa Mchungaji Mwamlima na Mwinjilisti Mwaibofu wa wa kanisa la Moravian. Mwili wa marehemu hakuingizwa kanisani kwa ajili ya kufanyiwa ibada ya mwisho. Moja kwa moja ikapelekwa Nonde, Mwamimwa akaendesha ibada huko. Ibada ilikuwa fupi Sana kuokoa muda ili asifufuke Tena.

Jeneza likashushwa huko kaburini, kwa namna ya kuvurumushwa.
Lile tipper ambalo lilikuwa na trip ya mawe, likabenua mawe yote Ndani ya kaburi.
Baada ya hapo vijana wakapiga posolo /chepe za kutosha kumfukia marehemu.

Huu msiba ulisisimua sana, watu wa Ghana, Mbata, Majengo, Nonde, Mabatini na hata Mwanjelwa walifika kuona mazishi hayo ya kigagula. Huyu Mama ndiye aliyekuwa anafanya mwanawe Jaili asikamatwe, na hata akikamatwa alikuwa anatoroka jela. Jaili alikufa miaka ya 1998/99 na kuzikwa Nonde.

Jaili ameishi maisha ya uzee kwa mateso makubwa, alikuwa anashinda Uhindini kwa Wahindi akiwaomba hela, wakimnyima anatishia kutoa Siri zao.

Mtoto wake aitwaye Manyenye alikuwa tishio Sana, naye alikufa siku chache baada ya kifo Cha baba Yake

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad