MSHAMBULIAJIwa Rayon Sports ya Rwanda, Mghana, Michael Sarpong, hana tatizo kuhusu kujiunga na Klabu ya Yanga lakini kuna masharti kadhaa inadaiwa kuwa uongozi unaomsimamia umeyatoa ambayo yanaonekana kuwa makubwa hasa katika masuala ya fedha.
Inadaiwa kuwa masharti ya dau lake la usajili ni Sh milioni 230 ili aweze kumwaga wino katika karatasi za mkataba wa timu hiyo ya Jangwani.
Sarpong, raia wa Ghana, kwa sasa amekuwa mchezaji huru baada ya Rayon kuvunja mkataba naye kufuatia madai ya kumshambulia rais wa timu hiyo katika vyombo vya habari vya nchi hiyo kufuatia kupunguziwa mishahara wachezaji kutokana na janga la Virusi vya Corona.
Mshambuliaji huyo mwenye uwezo wa kucheza winga zote mbili, amekuwa chaguo la kocha wa Yanga, Mbelgiji, Luc Eymael kutokana na tatizo la ukame wa mabao unaoendelea kwenye timu hiyo huku wakiwa wamewahi kufanya kazi pamoja.
Taarifa za uhakika kutoka nchini Rwanda, zinasema kuwa tayari Mkurugenzi wa Uendeshaji wa GSM, Injinia Hersi Said ameshamalizana na wakala wa mchezaji huyo licha ya kuwepo na utata juu ya dau la usajili wake.
Chanzo hicho kiliendelea kusema kuwa Yanga kupitia GSM ipo tayari kutoa kiasi cha dola 90,000 ambazo ni sawa na Sh milioni 207 lakini wakala wa mchezaji huyo, Mnyarwanda, Alex Kamanzi amewaambia Yanga watoe dola 100,000 (Sh milioni 230) ili kunasa saini ya nyota hiyo.
“Hilo dili lipo na linaweza kukamilika kwa sababu huyo kiongozi anayesimamia usajili Yanga ameshazungumza na wakala wa Sarpong kila kitu, yapo ambayo wamekubaliana na mengi bado hasa kwenye upande wa dau kwa sababu fedha waliyoweka mezani Yanga na wanayotaka wao imekuwa tofauti kidogo.
“Lakini kwa kuwa muda bado halafu mambo hayajakaa sawa kwa sababu ya Corona huenda wakafi kia pazuri na mchezaji akaja kucheza ligi ya Tanzania,” kilisema chanzo.
Championi Ijumaa lilimtafuta mshambuliaji huyo ambaye alikiri wakala kufanya mazungumzo na Yanga lakini akaomba amtafute wakala wake ndiye anaweza kutoa maelezo ya kutosha.
“Nimeambiwa juu ya hiyo dili na uzuri sasa anajua kila kitu lakini kwanza uzungumze na wakala wangu kwa sababu yeye ndiyo kila kitu katika hili jambo,” alisema Sarpong.
Championi Ijumaa halikuishia hapo ambapo liliweza kumpata wakala wa mchezaji huyo, Alex Kamanzi ambaye alisema: “Ni kweli tumekuwa na mazungumzo mazuri na Yanga juu ya mchezaji wangu ambapo yapo ambayo yanaweza kuwekwa wazi na ambayo hayawezi kuwekwa wazi ingawa pande zote mbili tunajaribu kuweka vitu sawa kwa faida ya pande zote.
”Mtego MBOWE Aliomtegea MAGUFULI Kwenye CORONA, Amenasa MWENYEWE, Ameigharimu CHADEMA” – NGEREZA