Mbunge wa Tarime Vijijini (Chadema), John Heche amesema na Mkurugenzi wa Mawasiliano, Itikadi, Uenezi na Mambo ya Nje wa Chadema, John Mrema wamemcharua Spika wa bunge Job Ndugai.
“Ndugai hizi ni kanuni zinazowataka wabunge wa Chadema kukichangia chama na wabubge kabla ya kugombea walizisoma na kuzikubali,” aliandika Mrema.
“Kumshambulia Mbowe kuwa michango ameagiza ni uongo. Aidha tuna taarifa za wabunge wa CCM na CUF kuchangia vyama vyao pia,” aliandika Mrema
Ndugai, hizi ni kanuni zinazowataka wabunge wa Chadema kukichangia Chama , na wabunge kabla ya kugombea walizisoma na kuzikubali. Kumshambulia Mbowe kuwa michango ameagiza ni UONGO.Aidha tuna taarifa za wabunge wa CCM na CUF kuchangia vyama vyao pia . pic.twitter.com/7V9b6eNVkn— Jon Mrema (@JonMrema) May 18, 2020
Mbunge wa Kilombero ( Chadema), Peter Lijualikali jana alisema kila mwezi Wabunge wa Chadema wanakatwa Sh. laki tano, eti kuchangia mfuko wa chama wakati wa kampeni, fedha zilipofika bilioni nane na walipohoji hizo fedha zipo wapi? Wakaambiwa uchaguzi ni harakati.Hivi mtu unajiunga na Chama hujui hata katiba ya Chama? Au unaungana na watesi wetu kufanya spinning za kijinga? Hakuna mtu anachangia chama hiki kinyume cha utaratibu wa katiba, elewa tu kwamba ulipata nafasi ya kugombea kwasababu waliokutangulia walichangia ujenzi wa chama. pic.twitter.com/ZrCSnRAM5A— John Heche (@HecheJohn) May 18, 2020
Nyie wote wana Twita Ni Wanufaika.
ReplyDeleteWaachieni Vidume waingie kazini.
Msajili wa vyama, Biswalo,Mbungo Halafu A.Ddiwani
Tanzania ni Salama na Haiko Mnadani.