Mrembo Alia Mastaa Bongo Kumpora Mzungu Wake..Ni Yule Aliyezidiwa Miaka 40 na Mumewe



DAR: Mrembo Aziza Mwakalukwa ‘Azzysuperstar’ ambaye ni msanii wa Bongo Fleva, amelia kutaka kuporwa mumewe, Wolf Gang ambaye ni Mzungu, raia wa Austria.

Aziza anayetamba na Wimbo wa Kamata, ameliambia Gazeti la IJUMAA kuwa, wanaotaka kufanya hivyo ni mastaa mbalimbali wa kike ambao hawaishi kumsumbua mumewe huyo kila kukicha.

Aziza ameolewa na Mzungu huyo miezi michache iliyopita ambaye wamepishana umri kwa miaka 40.

Alisema kuwa, baadhi ya mastaa wakubwa wa kike wamekuwa wakimuandikia mumewe ujumbe kupitia DM (Direct Messaging) ya Mtandao wa Instagram.

Aziza anasema mumewe huyo amekuwa akimuonesha kila kitu, hivyo anawajua hadi kwa majina.

“Unajua wanawake mastaa wa hapa Bongo sijui wakoje, wakiona mtu ana mume wake au hata mpenzi wake raia wa kigeni, mawazo yao yanakwenda mbali sana kwa sababu vichwani mwao wanafikiria kudanga tu,” amesema Aziza.

Aliendelea kusema kuwa, mastaa hao wanashindwa kuelewa kuwa hadi watu wanafikia hatua ya kuoana au kufunga ndoa, ni kwamba wameshibana na wamepita vikwazo vingi.

Msanii huyo alisisitiza kuwa, kama ataona tena tabia hiyo, atawachana laivu ili wajulikane ni nyakunyaku.

“Nimewavutia kasi tu. Pia watambue mapenzi siyo pesa, bali ni moyo, hivyo waache kujipendekeza kwa mume wangu. Mbona mwanzo walisema naolewa na mzee? Waniache kabisa,” amesema Aziza.

Aziza alitrendi mno kwenye mitandao ya kijamii baada ya kufunga ndoa na mumewe huyo kutokana na kuonekana ameolewa na mzee kupita kiasi, jambo ambalo analipinga kwa nguvu zote.

Mumewe huyo amekuwa akimsapoti katika kazi yake ya muziki.

Stori: IMELDA MTEMA, Ijumaa

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad