Msanii wa Filamu nchini, Jacqueliner Wolper, amesema ana wapenzi kama wanne kwa sasa ila anamuangalia mwenye tabia nzuri ndiye atakayemchagua kuwa naye.
“Huwa simuweke mjini mwanaume na sina kashfa ya kumuweka mwanaume mjini ninajijua mimi ni nzuri, msafi na ninajua kupika siwezi kufanya hivyo,” amesema Wolper
Msanii huyo amesema hana tabia ya kurudiana wala kuzungumza na wanaume zake alioachana nao.
Pia amesema hajawahi kupenda mume wa mtu kwa kuwa ana wivu katika mapenzi na anapenda kuwa na uhuru na mwanaume wake."Nina wapenzi kama wanne kwa sasa ila naangalia mmoja mwenye tabia njema ndiyo nitakuwa naye, simuweki mjini Meja Kunta na sinaga kashfa za kumuweka mwanaume mjini, ninajijua me mzuri, msafi, na najua kupika siwezi kufanya hivyo" - Jacqueline Wolper #Dadaz pic.twitter.com/idQgO5CEwR— eastafricatv (@eastafricatv) May 8, 2020
“Sina tabia ya kurudiana na wala kuongea na Ex wangu na sijawahi kupenda mume wa mtu maana mimi nina wivu napenda uhuru wa kuwa na mwanaume wangu,” amesema Wolper