Mshambuliaji wa msikiti Norway akana mashitaka



Raia mmoja wa Norway ambaye anatuhumiwa kwa kushambulia kwa risasi msikitini mjini Oslo mwezi Agosti mwaka uliopita na kumuuwa dada yake wa kambo amekana mashitaka yake yote, ikiwa kesi yake imeanza chini Norway.

Baada ya kusomewa mashitaka yake, Mwendesha Mashitaka Johan Overberg, mtuhumiwa Philip alisema halikubali hata kosa moja.

Kijana huyo wa umri wa miaka 22, inaelezwa alimpiga risasi nne dada yake wa kambo wa umri wa miaka 17, ambaye aliasiliwa kutoka China, na mwili wake ulikutwa Agosti 10, nyumbani kwake Baerum, magharibi mwa Oslo, ambapo siku hiyo hiyo kulifanyika shambulizi la msikitini.

Lakini hakuna mtu aliyepigwa risasi au kujeruhiwa katika kituo hicho cha Kiislamu cha msikiti wa Al-Noor.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad