Mwandishi wa habari wa kituo cha luninga cha CNN, mwenye asili ya watu weusi, Omar Jimenez amejikuta akitiwa mbaroni na jeshi la polisi wakati akiwa katika matangazo ya ‘Live’ yaliyokuwa yakionyesha maandamano ya baadhi ya watu kufuatia kifo cha George Floyd aliyefariki baada ya kukamatwa na polisi katika jimbo la Minnesota nchini Marekani.
Omar Jimenez alikuwa akitangaza mubashara huku akiwaonyesha baadhi ya waandamanaji waliyokuwa wamekamatwa na jeshi la polisi ghafla baadhi ya polisi wakamzunguka na kumuweka chini ya ulinzi bila kumpa sababu za wao kumkamata.
“Tunaweza kurudi mahali mnapopenda,” Jimenez aliwaambia polisi waliyokuwa wamevalia maski ya kuwakinga na gesi kabla ya mwandishi huyo ajajielezea mubashara kuwa yeye na timu yake ni sehemu ya waandishi wa habari.
”Hili ni miongoni mwa eneo ambalo doria imekuwa ikiendelea, kuangalia na kuwatawanya waandamanaji, ili watu waondoke eneo hilo,”- yalikuwa maneno ya mwandashi huyo kabla ya kukamatwa.
CNN imeripoti kuwa Gavana wa Minnesota, Tim Waltz amemuomba radhi rais wa chombo hicho cha habari, Jeff Zucker kwa kosa hilo na kusema kuwa walikuwa wanastahili kuwepo mahala hapo.