Mwanajeshi wa Ikulu Akutwa na Corona
0
May 08, 2020
RAIS wa Marekani, Donald Trump na Makamu wake, Mike Pence wamelazimika kupima tena maambukizi ya virusi vya corona baada ya mwanajeshi wa Ikulu ya nchi hiyo kubainika kuwa ana corona, vipimo vimeonesha Trump na Pence ni wazima.
“Tuna vipimo bora kuliko nchi yoyote duniani, nimepima jana na leo sina corona….” amesema Trump.
Taarifa ya Ikulu (White House) imesema pamoja na tukio hilo, rais na makamu wake wamefanyiwa uchunguzi wa afya zao na kukutwa wako katika hali njema
Tags