Mwanamke Amuua Mpenzi Wake Kwa Kutoosha vyombo

Mwanamke mmoja alifikishwa mahakamani Ijumaa,8,mei kwa kumdunga mpenzi wake hadi kufo kwa sababu alikataa kuosha vyombo baada ya kula.

Susan Njeri alidaiwa kumdunga mpenzi wake Kelvin Njenga mara ,11 na kisu baada ya kugombana nani ataosha vyombo.

Hakimu wa mahakama ya Milimani James wakiaga alisikia kuwa Kelvin alikuwa amemtembelea mpenzi wake Susan ili wajivinjari na hakufahamu kuwa labda hiyo ndiyo iliyokuwa siku yake ya mwisho duniani.

Upande wa mashataka ulisema kuwa Kelvin alimtembelea mpenzi wake tarehe 9 aprili, na kisha kumuua baada ya kula pamoja na kukosa kuosha vyombo, kitendo hicho kilifanyika katika eneo la tena estate Nairobi.


Hata hivyo akiwa mbele ya hakimu Wakiaga, Susan,25, alikataa madai hayo na kusema kuwa hana hatia yeyote,Aliomba mahakama kumuachilia kwa dhamana .

“I apply to be admitted to bond. Article 49 of the Constitution allows all suspects arraigned for any offence to be admitted to bond.” Susan Aliomba.

Kesi yake itasikizwa mei,14 ili mahakama iwao mahakama itaamua kumuachilia kwa dhamana au la.

Je unaweza kumuua mpenzi wako kwa kutoosha vyombo baada ya kula.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad