Mwanamuziki Rihanna Aingia Orodha ya Matajiri wa Uingereza



Mwanamuziki Robyn Rihanna Fenty (32) maarufu Rihanna kwa mara ya kwanza ameingia kwenye orodha ya Wanamuziki tajiri wanaoishi Uingereza na kushika nafasi ya 3. Amehamia London mwaka 2019

Rihanna ambaye pia ndiye Mwanamke wa kwanza kwa utajiri kwenye orodha hiyo ana utajiri wa takriban Tsh. Trilioni 1.325 (Paundi Milioni 468). Katika orodha hiyo amewapita pia wanamuziki kama Sir Elton John na Mick Jagger

Utajiri wake umekua kutokana na kufanikiwa kwa biashara yake ya vipodozi vya Fenty Beuty na kuingia ubia katika biashara nyingine kama 'Lingerie line' inayohusika na nguo za ndani na uuzwaji wa albamu zake 8 za muziki

Katika orodha hiyo, nafasi ya kwanza inashikiliwa na Sir Paul McCartney pamoja na Andrew Lloyd Webber ambao wote wana utajiri wa Paundi Milioni 800. Nafasi ya nne yupo Sir Elton John (£360m) na nafasi ya tano yupo Mick Jagger (£285m)

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad