aada ya Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam Paul Makonda kutangaza kutoa saa 24 kwa Wabunge waliopo mkoani kwake wakishindwa kuhudhuria mkutano wa Bunge jijini Dodoma.
Kumekuwa na maswali mengi ya kuwa RC Makonda yupo sahihi au hayupo sahihi.
Mwanasheria John Simon Kyashama ambaye pia ni Mchungaji wa Kanisa la River of Healing Ministry lililoko kiluvya kwa komba.
Amefafanua baadhi ya vifungu vya Sheria vinavyomruhusu na kumlinda Makonda kutokana na Tamko lake.
Sababu iliyopelekea kuongea ni baada ya kuona mijadala mitandaoni watu wengi wakikosea na kutafsiri sheria tofauti na kuamua kutoa ufafanuzi wa sheria kuhusu mjadala huo na tamko hilo la RC Makonda.